TCRA imesitisha utoaji Leseni Mpya za Maudhui Mtandaoni kwa muda
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesitisha utoaji wa leseni mpya za maudhui ya mtandaoni ili kujipa muda wa kufanya tathmini na maboresho ya utaratibu huo.
Kuna mabadiliko ya vifurushi kwenye mtandao wa Tigo ambayo yameleta malalamiko mengi kutokana na kuwa ya makubwa katika ushushwaji wa viwango vya GB ambavyo mtu anapata kwa malipo ya kwa siku, wiki na mwezi.
Kampuni ya Tecno kutoa zawadi kwa watakaoilipia simu ya Tecno Camon 16s mapema, yaani kufanya ‘pre-order. Simu ya Tecno Camon 16s inatarajiwa kuanza kupatikana sokoni hivi karibuni.
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ina nafasi pana tuu katika vita hii dhidi ya virusi vya Corona ambapo jitihada na nguvu nyingi vimewekwa hapa lakini kinachotoka bado kinakuwa na njia mbili!
Leo hii huwezi kuongelea Tanzania bila kuzungumzia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ambayo kimsingi ni taaluma kama zilivyo nyingine na mwaka huu tutapata kushudia tuzo za TEHAMA zinazoratibiwa/zitatolewa na TCRA.
Virusi vya Corona vimekuwa tishio kwenye mataifa mengi duniani ikiwemo Tanzania na hali hiyo imesababisha shughuli mbalimbali kusitishwa angalau kwa kipindi cha mwezi mmoja lakini janga hilo halijatuzuia kutumia vifaa vyetu vya kidijiti. Je, tutasalimika?
Dunia kote huduma zinarahisishwa zaidi kupitia teknolojia kwa sasa, na kampuni ya Azam Group haipo nyuma. Imekuja na app itakayotumika katika simu janja ili kumrahisishia mteja wake kuweza kununua na kufikishiwa bidhaa dukani kwake kwa njia rahisi na ya haraka zaidi.
Kampuni ya Helios Towers, inayojihusisha na uwekazaji na usimamiaji wa minara ya mawasiliano ya simu barani Afrika yajiingiza rasmi kwenye soko la hisa la jijini Landani, Uingereza.
Kampuni ya TALA inayokopesha kwa njia ya mtandao wa simu za mkononi, imetangaza kufunga shughuli zake Tanzania. Imetoa taarifa hiyo Jumanne Septemba 17, 2019 na kubainisha kuwa maelezo ya kina kuhusu uamuzi huo yatatolewa hivi karibuni.
Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA wametangaza kuja na kisimbusi kimoja kitakachoonyesha chaneli nyingi zaidi badala ya kuwa na kisimbusi (decorder) zaidi ya kimoja kuzipata zote.
Bunge la Tanzania kupitia spika wake Job Ndugai limetangaza kuendesha shughuli zake za vikao kwa njia ya mtandao kwa wabunge wote.
Mapendekezo ya sheria dhidi ya utumiaji usio sahihi wa laini za simu ambazo hazijasajiliwa yamefikishwa bungeni Tanzania.
Idadi ya watumiaji wa intaneti duniani imezidi kuongezeka na huku bara la Afrika likishika nafasi ya tatu kwa wingi wa watumiaji.
Wikiendi iliyopita kulikuwa na uzinduzi wa kitabu cha Riwaya jijini Dar es Salaam. Jina la kitabu linaenda kwa jina la Mimi na Rais. Hadi sasa unaweza ukawa unajiuliza kwa nini tuandike kuhusu kitabu katika kona ya teknolojia?
Umaarufu wa shirika la mawasiliano nchini Tanzania, TTCL umeongezeka mara dufu katika miaka miaka ya karibuni ukilinnganisha na muongo mmoja uliopita. Idadi ya watumiaji wa kadi za simu-TTCL inatazamiwa kuongezaeka baada ya kuwa ni LAZIMA kwa watumishi wa serikali kutumia mtandao huo wa simu.
Azam TV kuanza kuonesha chaneli za ndani bure ndani ya kipindi cha miezi 7. Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imetangaza kuwa Kampuni ya Azam tayari imepewa leseni kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inayoruhusu kurusha matangazo ya chaneli za bure.
Mataifa mengi duniani kila mara yanajitahidi kutumia mbinu za kisasa zaidi ili kuwezesha kulinda wanyama pori ambao wapo kwenye hatari ya kutoweka kutokana na vitu ambavyo wanavyo na vyenye thamani kubwa kutokana na kuuzwa kimagendo.
Habari za kuhusu usajili wa kadi za simu kwa njia ya alama za vidole hivi sasa sio habari mpya tena kwani tumekuwa tukikumbushwa na mitandao ya simu kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwenda kukamilisha zoezi hilo mara moja.
Wakazi wa Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela tarehe 02/05/2019 wameanza rasmi kutumia mfumo mpya wa Kielektroniki wa malipo ya ushuru wa maegesho ya magari (TARURA e-PARKING) ambao unatumia mfumo wa kielektroniki wa malipo ya serikali yaani Government Electronic Payment Gateway (GePG).