Chanzo kikuu cha mapato kwenye nchi yoyote ni kodi na kama hazikusanywi basi nchi hiyo itakuwa ndio mwanzo wa kuwa masikini. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imedhamiria kutanua wigo wa ukusanyaji kodi kwa kuwafikia wanaofanya biashara mtandaoni.
Hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan alikutana na wakuu wa mikoa wote nchini humo katika kikao cha kujadili mfumo wa anwani. Ni wazi kwamba teknolojia inakuwa nchini Tanzania na kuna mengi ambayo yamerahisishwa/kufanyika kwa wepesi kutokana na kukubaliana na mabadiliko hivyo kuchukua yale ambayo yanawezekana kwa sasa ili kuwa chachu ya kuleta maendeleo nchini humo.
Kitu kimoja ambacho watu wengi hawakukitegemea kukisikia kwenye mkutano huo uliofanyika mapema leo hii, Februari 8 2022 huko Dodoma ni wafanyabiashara mtandaoni kulipa kodi, kivipi? Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa nchi alisema:
………mifumo ya utambuzi ina tija kiuchumi na kijamii, na manufaa yake ni mengi ikiwa ni pamoja na kuwezesha kufanyika biashara mtandao, kuimarisha ulinzi na usalama lakini hata wanaofanya biashara mtandao tutawajua. Kwa sababu sasa hivi kuna biashara mtandao nyingi zinafanika na hazilipi kodi na hatuzijui lakini tutakapoingia mfumo huu tutawajua. Kila anayefanya biashara mtandao atasajiliwa, TRA itasoma, wapi itasoma kwahiyo watakwenda kudaiwa kodi zetu wazilipe ipasavyo.
Mfumo huu wa utambuzi ukuanza kutumika ni wazi kwamba utakuwa na athari kwa wateja kwa kmaana ya kwamba bei ya bidhaa husika zitapanda lakini pia tukumbuke kulipa kdo si dhambi bali fahari kwani fedha zitakazokusanywa zitumika kuleta maendeleo.
Vyanzo: ITV, mitandao mbalimbali
No Comment! Be the first one.