Utambulisho wa TAIC2022. Tanzania Annual ICT Conference (TAIC) ni Kongamano la wadau wa TEHAMA linalofanyika kila mwaka tangu mwaka 2017.
Kongamano hili huhusisha wadau kutoka sekta mbalimbali Tanzania na wanaokutana kwaajili ya kufanya majadiliano ya mwenendo wa TEHAMA nchini pamoja na kuweka mikakati ya namna ya kuboresha huduma za TEHAMA nchini.
Jana asubuhi Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA (ICT Commission) Dr. Nkundwe Moses Mwasaga alitangaza rasmi kufanyika kwa Kongamano la Mwaka la TEHAMA tarehe 26 – 28 Oktoba na litafanyikia Zanzibar. Mgeni Rasmi wa Mwaka huu atakuwa ni Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Kauli Mbiu ya Kongamano la Mwaka huu ni “Kutumia mabadiliko ya Kidigitali Katika Uchumi wa Bluu kwa Maendeleo ya Kijamii na Kiuchumi” .
Katika mkutano na waandishi wa Habari Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA alijibu maswali kutoka kwa waandishi wa Habari wa EFM, ZBC na Pugu Media. Aliwaelezea kuwa Tume ya TEHAMA ina wajibu wa kukuza TEHAMA nchini kwa kusajili kampuni ndogondogo za TEHAMA (Startups) pamoja na wabunifu mbalimbali wenye bidhaa au huduma ya TEHAMA na kuwakuza kupitia programu maalum ya SoftCenter.

Kongamano la mwaka huu ni la sita na majadiliano yatakayofanyika yatajikita katika kuzungumzia Kazi za Kidigitali (Digital Jobs), Majukwaa ya Kidigitali (Digital Platforms) na Miundombinu wezeshi, sera na mifumo ya kisheria (Enabling infrastructure, policy and legal frameworks).
Jisajili kupitia tovuti hii ili uweze kuhudhuria Kongamano la Mwaka la TEHAMA Mwaka huu #TAIC2022.
No Comment! Be the first one.