SWIFT ni nini na Urusi kutengwa kutumia huduma za SWIFT kuna maana gani?
SWIFT, au Society for Worldwide Interbank Financial Telecommunication, ni mtandao salama wa kimataifa wa kutuma ujumbe ambao benki hutumia kufanya malipo yanayovuka mipaka. Mtandao huo unarahisisha taasisi za kifedha kusambaza pesa kwa kila mmoja, na kusaidia kuhakikisha kuwa biashara za kimataifa inaendelea vizuri.