Kwa sasa ni kama watu wameamka, hii ni moja ya mtazamo wa mteja (customer experience) ambao nimekutana nao katika tafiti zangu nikiwa nafikiria ni simu gani bora yakuendana na matumizi yangu.
Infinix Note 12 G88 | Samsung Galaxy A14 |
Display/Ukubwa: Inchi 6.7 (AMOLED) | Display/Ukubwa: Inchi 6.6 (PLS LCD) |
Kamera: Zipo tatu, kamera kuu ni MP 50
Selfi Kamera: MP 16.0 Video: 2K (2,048X1,080) @30fps |
Kamera: Zipo tatu – ya MP 50.0, MP 5.0 na MP 2.0.
Selfi Kamera: MP 13.0 Video: FHD (1920×1080)@30fps |
Betri: mAh 5000 | Betri: mAh 5000 |
RAM: Toleo la GB 4 na la GB 6 | RAM GB 4 |
Hapo awali watu wengi waliamini Samsung ni simu bora zaidi lakini sasa wakati una mabadiliko kuna vitu vya kuzingatia kwenye ununuzi wa simu, kwa mfano natumia kifaa cha Infinix Note 12 na nina furaha nacho zaidi, ni rahisi kutumia na chapa ya kudumu kama hii.
“Imebadilisha mtazamo wangu kuhusu chapa ya simu mahiri, kadiri muda unavyopita nadhani watu zaidi wataelewa hili kama vile nilivyoelewa kampuni nyingi zinakuja na simu nzuri na gharama inatupendelea sisi wateja ni juu yetu kuwa makini na maamuzi yetu”
”Lakini kile kilichodanganywa kama mtazamo wa zamani sio tena, tuna brand nzuri zaidi kama Infinix sasa ambayo inakuja na muundo mzuri, kamera na bei nafuu na chapa yenyewe inavutia zaidi kuwa nayo, Infinix Note 12 yangu ina vitu vingi zaidi kulinganisha na Samsung ya kaka yangu A14,.
Tulizinunua kwa wakati mmoja lakini yangu inachaji kwa haraka zaidi ya 33W inachaji haraka, skrini yake ni kubwa zaidi hivyo nafurahia zaidi kutazama na kucheza game kwenye simu yangu kulinganisha.
Na yake nabaki kumcheka alichagua simu yake kwa sababu alidhani itakuwa nzuri lakini amekosea kabisa, inachukua muda mrefu kuchaji kikamilifu na hawezi kucheza gemu kubwa kwa sababu ya Ram yake kuwa ndogo 4GB tu”.
Ni wazi kwa sasa kuna chapa nyingi sana za simu janja ambazo zinagfanya vizuri katika soko. Kwa mwaka huwa zinatoka simu nyingi sana lakini ili ubakie na ile ileyo bora inabidi uhakikishe unachagua ile yenye sifa (specification) nzuri kulingana na bei.
Ni mara nyingi watu wamejikuta wakinunua simu au vifaa vingine vya kielektroniki kwa sababu ya chapa (brand) na sio kwa ajili ya sifa za undani ambazo zinakuja na vifaa hivyo, ni bora kuangalia uwezo au sifa za kifaa kabla ya kukinunua.
Je watumiaji wa simu hizi mnalipi na kusema kuhusiana na ushuhuda huu?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.