fbpx

Mfumo wa kuhakiki mtu kwa mishipa ya mkono wadanganyika

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Sababu mbalimbali za kiusalama zinafanya wataalam waweze kubuni njia ya kutumia ili kuhakikisha kifaa/mahali fulani panakuwa salama.

Sio kitu cha ajabu/kushangaza kuona vifaa mbalimbali vikitumia teknolojia ya alama za vidole, utambuzi wa sura katika kuweza ulinzi madhubuti lakini katika teknolojia ya karibuni kabisa inayotumia utambuzi wa mishipa ya mkono imekubali kudanganyika!.

Mfumo wa utambuzi wa mishipa ya mkono unavyofanya kazi.

Katika njia ya kukabiliana na ulinzi madhubuti upo mfumo wa utambuzi wa mishipa ya mkono husika ambapo inatumika kompyuta kuangalia/kuhakiki umbo, urefu na mishipa ya mkono husika kitu ambacho kinafanyika kila mara ambapo mhusika atataka kuingia sehemu hiyo.

INAYOHUSIANA  Udukuzi WhatsApp: Udukuzi mkubwa umefanyika kwa watumiaji wa WhatsApp

Ilikuaje mfumo wa kuhakiki mishipa ya mkono ukadanganyika?

Wadukuzi walipiga picha za mkoni takribani 2500 kwa kutumia kamera iliyokuwa imeondolewa kifaa fulani ili kuweza kupata picha nzuri ya mishipa kisha wakaenda kutengeneza mkono wa bandia na kuweka taarifa za mishipa kwenye kitu hicho walichotengeneza.

kuhakiki

Teknolojia mpya ambayo inaweza kutambua mishipa ya mkono ili kutoa idhini kitu/mahali fulani pafunguke.

Teknolojia ambayo mtu akifikiria njia ya kukabiliana na kitu fulani wapo watu wengine pia wanasugua vichwa vyao kuweza kutafuta udhaifu wa kile ambacho kipo.

Vyanzo: Engadget, VICE

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.