Utengenezaji na Uuzaji wa simu janja ni moja kati ya soko kubwa sana na mara kwa mara tumeshuhudia makampuni mengi yakijipatia faida kubwa.
Makampuni kama Apple na Samsung mara kwa mara wameonekana wakichuana jino kwa jino katika kuhakikisha kuwa nani anabaki kuwa juu katika soko la kutengeneza na kuuza simu janja.
Kingine ni kwamba kwa sasa hakuna uhitaji mkubwa sana kwa watumiaji wa simu janja kwa wakati huu— yaani kitaalam ni kwamba watu hawana uhitaji wa simu mpya ukaichana na wanazotumia.
Hali kama hii mara nyingi huwa inasababishwa na mambo mengi lakini lile la haraka haraka ni kwamba labda matoleo mapya yanakua hayana kitu kipya chenye tija ukilinganisha na matoleo ya zamani.
Kwa miaka mingi Samsung imekua ikiongoza katika kuuza idadi kubwa sana ya simu janja huku ikiwa inafuatiwa na kampuni ya Apple wenye iPhone.
Lakini hii haina maana ya kwamba Apple hawajawahi kushika usukani katika hili hata wao mara kadhaa wamewatoa jasho wapinzani wao.
iPhone 14 zilivyotoka tuu Apple ndio walikua kileleni kama waongozaji katika soko ambao wameuza simu nyingi lakini kwa sasa Samsung wamepindua meza.
Kwa mujibu wa tafiti ambayo imefanywa na kampuni ya Canalys umeonyesha wazi ukuaji na uporomokaji wa mauzo ya simu kwa idadi.
Tafiti hiyo imeyagawa makampuni katika vipingi viwili yaani robo ya kwanza ya mwaka na robo ya tatu ya mwaka kuanzia mwaka 2020 mpaka 2023.
Makampuni nguli kama Vivo, Xiaomi, Oppo, Apple Na Samsung yanahusishwa katika orodha hii huku kwa robo ya kwanza ya mwaka huu Samsung akiongoza.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je unahisi ni kweli siku hizi ununuzi wa matoleo mapya ya simu umepungua ukilinganisha na zamani?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.