Kutengeneza iPhone yako mwenyewe – Apple kuuza vipuri na mafunzo ya matengenezo mbalimbali
Apple kuja kukuruhusu kutengeneza iPhone yako mwenyewe iwapo imeharibika. Uwezo huo umetangazwa na Apple ambapo wamesema wataanza kuuza vipuri mbalimbali kama vile betri, kioo (display) na kamera za iPhone na baadae kuanza kuuza hadi vipuri vya kompyuta za Macbook.