Nawezaje kurudisha WhatsApp yangu? – Hili ni moja la swali ambalo tumekuwa tukilipata sana kutoka kwa wasomaji wetu. Kumekuwa na ukuaji wa tatizo la kufungiwa akaunti za WhatsApp hasa kwa watumiaji wa simu za Android, na mara nyingi umehusisha na utumiaji wa apps zisizo rasmi.
Ingawa tayari tumeshaandika na kutoa sababu kwa nini tunakushauri usitumie matoleo ya apps yasiyorasmi, ila leo tutakupa njia ambayo bila kujali sababu ya akaunti yako kufungiwa ni njia ambayo inaweza kukusaidia kupata tena kutumia akaunti yako ya WhatsApp kama kawaida – kupitia app rasmi au mbadala.
Sababu zinazopelekea kufungiwa akaunti ya WhatsApp.
- Kutumia toleo lisilo rasmi la WhatsApp. Kuna matoleo mengi yasiyo rasmi ya WhatsApp yanayopatikana mtandaoni, lakini matoleo haya huwa ni matoleo ambayo yanaenda kinyume na hakimiliki na taratibu za kiusalama za WhatsApp, utumiaji wa apps hizi unakupa sifa ya kukiuka masharti ya huduma ya WhatsApp. Ikiwa unatumia toleo lisilo rasmi la WhatsApp, akaunti yako inaweza kupigwa marufuku.
- Kutuma jumbe nyingi (broadcast) au ujumbe usioombwa. WhatsApp ina sera kali dhidi ya kutuma jumbe nyingi kwa wakati mmoja, hasa kwa watu ambao hawajahifadhi (save) namba yako. Kama wapokeaji kadhaa wa ujumbe wakisema ujumbe wako hawakuuomba, basi akaunti yako inaweza kufungiwa (banned).
- Kueneza habari zisizo sahihi au propaganda. WhatsApp inapigania sifa ya kuwa jukwaa salama kwa watumiaji wake, na salama kwaa mawasiliano. Ikiwa utapatikana ukieneza habari zisizo sahihi au propaganda, akaunti yako inaweza kupigwa marufuku.
- Kuvunja masharti mengine ya huduma. WhatsApp ina masharti mengine ya huduma ambayo watumiaji lazima wakubaliana nayo. Ikiwa unavunja masharti yoyote kati ya haya, akaunti yako inaweza kupigwa marufuku. Kuyafahamu zaidi tembelea – > WhatsApp Terms.
Jinsi ya Kurudisha Akaunti Iliyopigwa Marufuku ya WhatsApp
Ikiwa unaamini kuwa akaunti yako ya WhatsApp imepigiwa marufuku kwa makosa, unaweza kujaribu kuirejesha kwa kufuata hatua hizi:
Omba ukaguzi kupitia app yao.
- Fungua WhatsApp na gonga kwenye dots tatu kwenye kona ya juu ya kulia.
- Kisha, chagua “Settings” > “Account” > “Privacy” > “Account status” > “Request a review.” Utaulizwa kuingiza nambari ya usajili ya nambari 6 inayotumwa kwako kwa SMS. Mara tu utakapoingia nambari, unaweza kuwasilisha ombi lako la ukaguzi.
- Wasiliana na WhatsApp support. Ikiwa haukupata jibu la ombi lako la ukaguzi ndani ya masaa 24, unaweza kuwasiliana na WhatsApp support. Unaweza kupata maelezo ya mawasiliano ya WhatsApp support kwenye tovuti yao. – Tembelea Contact WhatsApp
- Wakati wa kuwasiliana na WhatsApp support, hakikisha kuwapa taarifa zifuatazo:
- Jina la mtumiaji wa WhatsApp
- Nambari yako ya simu
- Tarehe na saa akaunti yako ilipopigwa marufuku
- Maelezo mafupi ya kwa nini unaamini akaunti yako imepigiwa marufuku kwa makosa
- Ikiwa WhatsApp support inakubali kwamba akaunti yako imepigiwa marufuku kwa makosa, wanaweza kuifungua tena. Lakini, hakuna uhakika kwamba watafanya hivyo na kufanikisha.
Mfano wa Jumbe za Kuomba Ukaguzi
Hapa kuna ujumbe wa sampuli unazoweza kutumia kuomba ukaguzi wa akaunti yako ya WhatsApp iliyopigwa marufuku, kumbuka kufanya mabadiliko yeyote unayoweza kufanya ili ujumbe wako uwe wa kipekee na kitofauti:
Ya kwanza:
Hi WhatsApp,
I am writing to request a review of my banned account. I believe that my account was banned in error, as I have never used any unofficial versions of WhatsApp or engaged in any prohibited activities.
I have been a loyal WhatsApp user for many years and have always found the app to be reliable and user-friendly. I am very disappointed that my account has been banned, as I use it to stay in touch with friends and family all over the world.
I would be grateful if you could review my account and restore it as soon as possible. I can provide you with any additional information that you may need.
Thank you for your time and consideration.
Ya pili:
Dear WhatsApp,
I am writing to request a review of my banned account. I believe that my account was banned in error, as I have never used any unofficial versions of WhatsApp or engaged in any prohibited activities.
I have been using WhatsApp for over 5 years and have always found it to be a valuable tool for communication. I use it to stay in touch with friends, family, and colleagues all over the world.
I am very disappointed that my account has been banned, as it has caused me a great deal of inconvenience. I am unable to communicate with my loved ones and I am also unable to use WhatsApp for work.
I would be grateful if you could review my account and restore it as soon as possible. I can provide you with any additional information that you may need.
Thank you for your time and consideration.
Soma maujanja mengine hapa – Teknokona/Maujanja
Ikiwa akaunti yako ya WhatsApp imefungiwa, itakubidi kuwa na subra. Ni tatizo ambalo mhudumu anaweza litatua kati ya muda wa masaa 4 hadi 24. Ila tupo pazuri. Nitacoordinate kesho ili upate an update,
No Comment! Be the first one.