China safari hii imekuja kivingine, kwa sasa imetoa tamko kuwa waandaaji wa App (developer) wawe wametokea China au zihusishe ubia na kampuni au wananchi wa nchini China.
Kingine cha msingi ni kwamba waandaaji hao wa App wanatakiwa kuweka anuani zao na taarifa za muhimu kuhusiana na biashara hiyo.
Kumbuka China kipindi cha nyuma imekua ikizua App ambazo zinafanana na ChatGPT na magemu kulazimika kuwa na kibali maalumu, na sasa wamekuja na matakwa mapya kwa watengenezaji wa apps.
Wizara ya Viwanda na Taarifa –Ministry of industry and information (MIT)—kwamba watengenezaji wa App wote lizima wajaze taarifa zao za biashara na kujiandikisha kufikia Machi 2024.
Baada ya muda huo ni kwamba serikali hiyo itaanza kuchukua taratibu za kuwaadhibu watengenezaji wa App ambao hawatakuwa wamefuata utaratibu huo, lakini hawakuweka wazi juu ya hatua za adhabu zitakazochukuliwa.
Watu wanajiuliza je itakua ni kuzitoa App hizo App Store au ni kuwatoza faini au vyote kwa pamoja? Lakini mpaka sasa majibu hayapo wazi.
Kwa haraka haraka ni kwamba mkazo huu unawaathiri wale waandaaji App wadogo wadogo wa kujitegemea au hata wale ambao wana App za mlengo wa kisiasa.
Wengi wanahisi kwamba labda serikali imefanya hivyo kusudi kwa sababu ina mpango wa kuzuia App za mitandao ya kijamii kama vile Twitter/X, Instagram, na Facebook. Kumbuka tayari kuna vita kubwa ya kiteknolojia inayoendelea kati ya Marekani na Uchina, ikihusisha vikwazo mbalimbali vya kiteknolojia na bidhaa.
Ningependa kusikia kutoka kwako,niandikie hapo chini katika eneo la comment je hii wewe umeipokeaje? Unadhani ni sawa kwa vikwazo/mkazo huo uliowekwa kwa waaandaji wa App?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.