fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
AI apps Intaneti Kompyuta simu Teknolojia Uchambuzi

Teknolojia Mpya zitakazotumika sana mwaka 2022

Teknolojia Mpya zitakazotumika sana mwaka 2022
Spread the love

Unafahamu teknolojia mpya zitakazotumika sana mwaka 2022? Teknokona leo tunakuletea orodha ya teknolojia mpya zinazotarajiwa kutumika kwa wingi katika shughuli mbalimbali kuanzia mwaka 2022 na kuendelea. Orodha hii itajikita zaidi katika teknolojia za habari na mawasiliano pamoja na ukusanyaji, utumaji na uchakataji wa taarifa (data).

Teknolojia ya habari na mawasiliano imekuwa kwa kasi sana katika kipindi cha miaka kumi iliyopita na mpaka sasa tumeweza kushuhudia matumizi mbalimbali ya teknolojia hizi kama kasi ya utumaji wa taarifa kukua ndani ya miaka kumi kutoka 3G mpaka 5G. Teknolojia mpya zitakazotumika sana mwaka 2022 ni pamoja na:

Akili Bandia (Artificial Intelligence): Akili Bandia ni uigaji wa michakato ya akili ya binadamu na mashine kwenye mifumo ya kompyuta. Programu za Akili bandia huzingatia stadi tatu za utambuzi ambazo ni kujifunza, kufikiria na kujisahihisha. Mifumo ya Akili bandia hufanya kazi kwa kuchukua kiasi kikubwa cha data, kuzichanganua data kwa uwiano na ruwaza (patterns), na kutumia ruwaza hizi kufanya ubashiri kuhusu hali za siku zijazo. Mfano wa matumizi ya Akili bandia ni kama Google search(utafutaji wa kitu Google) ambapo Google italeta majibu kulingana na eneo ulipo, vitu unavyopendelea na mada ulizowahi kutafuta.

SOMA PIA  Yahoo: Yaibiwa Anuani na Maneno ya Siri kwa Barua Pepe!

Teknolojia Mpya

5G: Ni kiwango kipya cha kimataifa cha mtandao usiotumia waya baada ya mitandao ya 1G, 2G, 3G na 4G. 5G huwezesha aina mpya ya mtandao ambayo imeundwa kuunganisha kila mtu na kila kitu pamoja, ikijumuisha mashine, vitu na vifaa. 5G pia Imeundwa kuwa na uwezo mkubwa ili kuwezesha matumizi ya watumiaji wa kizazi kijacho, kuwezesha miundo mipya ya mifumo na kutoa huduma mpya. Matumizi ya teknolojia ya 5G ni pamoja na kuboresha uwezo wa magari kujiendesha, kuboresha uzalishaji wa bidhaa viwandani na pia kuboresha mawasiliano kati ya vifaa vya kielektroniki.

Teknolojia Mpya

Picha: Muonekano wa matumizi mbalimbali ya 5G

Uhalisia Pepe (Virtual Reality): Ni uigaji wa mazingira unaoweza kufanana au tofauti kabisa na ulimwengu halisi. Mtu anayetumia kifaa cha uhalisia pepe anaweza kutazama ulimwengu wa bandia, kuzunguka ndani yake, na kuingiliana na vipengele au vitu pepe. Kuna maeneo mengi ambayo teknolojia ya uhalisia pepe inaweza kutumika ikiwemo elimu, usanifu wa majengo na miji, uhandisi, burudani, sanaa, huduma ya afya na matibabu, sayansi ya kijamii na saikolojia.

Teknolojia Mpya

Picha: Muonekano wa kifaa cha Uhalisia pepe (Virtual Reality)

Cloud Computing: Ni utoaji wa huduma mbalimbali kupitia mtandao. Nyenzo hizi ni pamoja na zana na programu kama vile hifadhi ya data, seva, mitandao na programu. Badala ya kuweka mafaili kwenye diski unayomiliki unaweza kutumia ‘Cloud-based storage’ itakayokuwezesha kuhifadhi mafaili kwenye hifadhidata ya mbali. Maadamu kifaa chako cha kielektroniki kinaweza kuwasiliana na tovuti hiyo kinaweza kufikia data na programu za kukiendesha.

Teknolojia Mpya

Picha: Baadhi ya huduma zinazotolewa kupitia Cloud Computing

Endelea kutembelea tovuti yetu kufahamu zaidi kuhusu teknolojia na matumizi yake na pia kupata habari mbalimbali za kiteknolojia. Soma makala zetu zingine hapa.

Semu Msongole

Digital Marketing Strategist, Content Writer, and Social Media Manager at Teknokona Blog.

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania