Kama kuna nchi yenye sheria kali za mitandaoni basi Uchina ni moja kati ya nchi hizo. Hata kama haiwezekani kuingilia ujumbe kati ya mtu na mtu lakini kuifungia inawezekana ๐ ๐ ๐ ๐ .
WhatsApp ni app iliyo maarufu duniani kote imejikuta katika wakati mgumu baada ya serikali ya nchini Uchina kufanikiwa kuzuia mawasaliano ya app hiyo maarufu. Hii inalenga kuzidi kuzuia mazungumzo ya usiri baina ya watu kabla ya mkutano mkuu wa chama (China Communist Party) kinachoongoza nchi hiyo.
Huduma za kuchati kama vile WeChat ambayo pia ni maarufu sana nchini humo, zinaendelea kupata baraka za serikali kwa kuwa zinaruhusu serikali ya nchini humo kupata data za watumiaji wa app zake kwa urahisi. Hali ni tofauti kwa WhatsApp ambapo teknolojia ya mawasiliano inayotumia inahakikisha usiri na usalama wa mawasiliano ya watumiaji wake.
Wananchi wengi wa Uchina wanatumia zaidi WhatsApp kuliko sms za kawaida kwa sababu app hiyo hairuhusu ujumbe wa mtu na mtu kusomwa na mwingine isipokuwa kati ya mtu/watu wanaowasiliana tu.
Tatizo la WhatsApp kutofanya kazi lilianza leo (Sept. 26) ambapo mtu hawezi kutuma ujumbe wa picha/maneno au hata sauti.

Nchi mbalimbali ikiwemo Uchina imekuwa zikilazimisha makampuni yanajihusisha na masuala ya teknolojia kuhifadhi data za wateja wao katika nchi husika. Zipo kampuni zilizotekeleza agizo hilo ila kampuni kama Google imekaidi agizo hilo na kuamua kutofanya kazi kabisa nchini Uchina.
Mwezi Julai, Apple iliondoa kwenye soko lake la apps programu tumishi ambayo iliwezesha mtumiaji kuingia kwenye tovuti yoyote nchini Uchina (hata kama imefungiwa).
Kudhibitiwa kwa WhatsApp kunatokana na kwamba Uchina inakaribia kufanya mkutano mkuu wa chama (Oct. 18) hivyo mamlaka husika haihitaji mkanganyiko wa habari lakini pia WhatsApp hairuhusu jumbe za watu kusomwa na wengine (end-to-end encryption).
Vyanzo: Telegraph, mitandao mbalimbali