fbpx

Bill Gates asema anatumia simu ya Android, Ni samsung Galaxy S8?

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Katika mahojiano ya hivi karibuni na Fox News, Mwenyekiti wa Microsoft na tajiri namba moja duniani Bill Gates, amebainisha kuwa amebadili simu na sasa anatumia simu yenye mfumo wa Android.

“Hivi karibuni nimebadili kwenda Simu ya Android yenye wingi wa programu za Microsoft”, alisema katika mahojiano hayo.

Aliendelea kusema kuwa, “Lakini ushindani katika programu na IT nafasi ambayo steve (Jobs) alisaidia kukuza ni jambo la ajabu sana. Na microsoft ni sehemu kubwa ya hilo. Imekuwa ni sekta ya miujiza ambayo yeye na mimi tuliifanyia kazi”

Bill Gates asema anatumia simu ya Android

Bill Gates asema anatumia simu ya Android

Haijulikani ni simu gani ya Android anayoitumia Bill Gates katika shughuli zake za kila siku, lakini inadhaniwa kwamba anatumia Samsung Galaxy S8 toleo maalum la Microsoft Edition ambalo lilizinduliwa mwezi April mwaka huu.

INAYOHUSIANA  Arrow Launcher sasa kujulikana kwa jina la Microsoft Launcher

Mke wake, Bi Melinda Gates alishasema ya kwamba nyumbani kwao hakuna kabisa bidhaa za Apple, ata watoto wao wanatumia bidhaa zingine lakini si za Apple.

Simu hiyo inapatikana katika maduka mengi ya Microsoft na ambayo ina programu/apps nyingi za Microsoft.

Samsung Galaxy S8

Uchaguzi wa Gates kutumia Android unaonekana wenye kumfaa zaidi kwa kuzingatia Android ina mfanano na Microsoft ambayo yeye ndiye sehemu ya uundaji wake.

INAYOHUSIANA  Ndege yacheleweshwa kutokana na 'Hotspot' yenye jina la Galaxy Note 7

Kutumia Android kwa Bill Gates ni kwa sababu ni mfumo wa wazi ambao unamfanya aweze kufanya anachotaka tofauti na mfumo wa iOS ambao umefungwa.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.