Program ya Google slides imezidi kujaribu kuwavutia watumiaji baada ya kuleta uwezo wa wasikilizaji kuweza kuuliza maswali moja kwa moja kwa njia ya mtandao.
Hatua hii inaonesha hatua za wazi kutoka katika kampuni hiyo kupambana na kampuni ya Microsoft ambayo nayo inatoa huduma kama hiyo kwaajiri ya presentations.
Jaribu kufikiria ungekuwa unawakilisha maada kwa wasikilizaji wanaokaribia mia moja, ni wazi katika hali kama hiyo ni ngumu kupokea maswali kutoka kwa wasikilizaji na kuyajibu hii inatokana na ukweli kwamba pamoja na mambo mengine kuna wasikilizaji ambao wanaona haya kuuliza maswali kukiwa na watu wengine.
Katika blogu yao Google wanasema huduma hiyo mpya ambayo imepewa jina la Slides Q&A itasaidia watoa mada duniani kote kuweza kujua hali halisi ya juu ya jinsi maada zao zinavyopokelewa na wasikilizaji na pia njia hii itawapatia wasikilizaji wa mada nafasi ya kuuliza maswali kuhusu kinachofundishwa ama kuongelea moja kwa moja.
Katika slides kutakuwa na link nyepesi ambayo itakuwa inaonekana na watumiaji wataweza kuuliza maswali ama kutoa maoni juu ya maada kwa kuifungua link hiyo katika simu zao ama Laptop zao.
Pamoja na yote kwa kutumia link hiyo wasikilizaji wanaweza pia kupiga kura juu ya swali ambalo wengi wanaliafiki na hiii inaweza kumsaidia mtoa mada kuweza kutilia mkazo kwa swali ambalo linaulizwa na wengi.
Kimsingi haya ni mageuzi yenye maana saana katika namna ambayo tumekuwa tukiwasilisha mada kwa kutumia Powerpoints karibu kwa muongo mmoja, njia hii itawaleta karibu zaidi watoa mada na wasikilizaji kitu ambacho hakikuwepo hapo kabla.