Mwanamke mmoja amenusurika adhabu kari ya kifungo cha maisha jela baada ya kukutwa na kosa la kujaribu kumuuza mtoto wake kupitia mtandao.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 20 aliweka tangazo la kumuuza mtoto wake kupitia tovuti ya matangazo madogo madogo ya Gumtree mwishoni mwa mwaka jana. Inasemekana watu walipoliona tangazo hilo walilitaarifu jeshi la polisi la nchi hiyo.
Alikuwa anamuuza mtoto wake kwa takribani dola 340 za kimarekani (Rand 5,000 | Tsh 745,000 | Ksh 34,000). Kwa sasa mtoto huyo analelewa na watu wa ustawi wa jamii.
Katika utetezi wake mama huyo alidai kufikia kufanya maamuzi hayo kutokana na mpenzi wake aliyekuwa anatoa pesa za matunzo ya mtoto huyo kuacha kufanya hivyo baada ya kufanya vipimo vya DNA na kugundua mtoto huyo si wa kwake kama alivyokuwa anafikiri.
Kutokana na hilo amekuwa katika wakati mgumu kifedha na hivyo akaamua bora kumuuza mtoto huyo apate kulelewa na wanaoitaji mtoto. Mtoto alikuwa na umri wa miezi 19 wakati huo.
Kutokana na hilo mahakama moja nchini humo ikampa kifungo cha miaka 3 cha nje, atatakiwa kukaa nyumbani tuu, kushiriki katika ushauri wa kisaikolojia na kazi za jamii.
Duhhh… una mtazamo gani juu ya hili?
Vyanzo: iol.co.za na mitandao mbalimbali