fbpx
Intaneti, Kompyuta, Maujanja, Teknolojia, Windows 10

Namna ya kuzima ‘Automatic update’ kwenye Windows 10

namna-ya-kuzima-automatic-update-kwenye-windows-10
Sambaza

Kwa mujibu wa Microsoft ni kwamba toleo la Windows 10 litakuwa linapokea masasisho (updates) kwa njia ya moja kwa moja. Njia hiyo imekuwa ikitumika kwa baadhi ya matoleo ya nyuma ya Windows.

Masasisho hufanyika kwa ajili ya kuboresha au kurekebisha pale penye upungufu katika toleo la Windows. Masasisho ya Windows yanatumia njia ya Intaneti hivyo mwenye kompyuta anahitaji kuwa na kiwango kikubwa cha kifurushi cha intaneti.

Hatua hii kwa wengine ambao hawahitaji masasisho hayo huwa ni kero hasa pale wanapokuwa na kiwango kidogo cha data ambacho wamekusudia kutumia kwa matumizi mengine na si kwa ajili ya masasisho.

Hali hii kwa wengi imekuwa ni kero na usumbufu kwa kuliwa data zao. Leo kupitia tovuti yako ya teknokona tutakuelekeza namna ya kuzima automatic update katika windows 10. Katika makala haya tutakuelekeza njia mbili za kufanikisha zoezi hili.

Njia ya kwanza

1. Washa Kompyuta yako na katika search andika “service” kisha bonyeza enter,
2. Itafunguka menu tafuta “Windows Update”. Ukishaipata bonyeza mara mbili (double click),
3. Itafunguka menu nyingine na utafungua palipoandikwa Startup type na utaona Automatic (Delayed Start), Automatic, Manual na Disabled; hakikisha unachagua Disable na unabonyeza Apply>OK.

INAYOHUSIANA  Kurasa za Mark Zuckerberg zadukuliwa, je wewe upo salama?
Habari Picha: Hatua ya kwanza.
Habari Picha: Hatua ya pili.
Habari Picha: Hatua ya tatu.

Njia ya pili

1. Fungua RUN kwa kubonyeza Windows key pamoja na R (Windows key + R)
2. Andika “gpedit.msc” kisha bonyeza OK
3. Itafunguka menu ya “Group policy editor”
4. Fungua “Administrative Templates” iliyo chini ya “Computer Configuration”
5. Kisha fungua “Windows components”
6. Fungua “Windows Update”
7. Fungua kwa kudouble click “Configure Automatic Updates”
8. Kisha chagua Disable Automatic Updates>OK

Habari Picha-Njia ya pili: Hatua ya kwanza.
Habari Picha-Njia ya pili: Hatua ya pili.
Habari Picha-Njia ya pili: Hatua ya tatu.
Habari Picha-Njia ya pili: Hatua ya nne.
Habari Picha-Njia ya pili: Hatua ya tano.
Habari Picha-Njia ya pili: Hatua ya sita.

Kwa njia hizo mbili tulizozionesha ukitumia moja kati ya hizo utaweza kufanikisha kuzuia Auotomatic update kwenye Windows 10. Lakini njia nzuri ambayo tunakushauri kuitumia zaidi na kama haina usumbufu kwako ni ya pili.

INAYOHUSIANA  Google I/O - Apps za Android ktk Chrome OS, Toleo la Android 7 na habari nyingine!

Kama ukitaka kurudisha kama ilivyokuwa mwanzo fuata njia hizo na uondoe hiyo disable na utapata masasisho kama kawaida kwa namna utakavyoletewa na Microsoft wenyewe. Usisite kutupa maoni yako au maswali kuhusiana na makala hii.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.