fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

apps Teknolojia YouTube Shorts

Dola milioni 100 kutolewa kwa watumiaji wa YouTube Shorts

Dola milioni 100 kutolewa kwa watumiaji wa YouTube Shorts

Spread the love

Kama njia mojawapo ya kuvutia watumiaji wa “Mdogo wake” YouTube kampuni hiyo imepanga kugawa jumla ya dola za Marekani zipatazo milioni 100 kwa watumiaji mbalimbali wa YouTube Shorts.

Kama njia ya kuongeza motisha kwa watu YouTube imejipanga kutumia kiasi kikubwa cha pesa kwenda kwa watu mbalimbali kutokana na kile ambacho wamekuwa wakikiweka kwenye YouTube Shorts lakini tuulizane swali rahisi tuu je, unafahamu pacha huyo wa tovuti hiyo mahususi kwa ajili ya machapisho yaliyo katika mfumo wa picha na sauti?

YouTube Shorts ni sehemu ya YouTube ambayo ambapo ili picha mnato iweke kwenye kundi la “Shorts” basi ni LAZIMA chapisho husika lisizidi sekunde 60 au chini ya hapo. Mtengenezaji wa picha jongefu HAITAJI wanamfuatilia au waliangalia machapisho yake kuweza kutengeneza YouTube Shorts.

Sasa YouTube wametenga kiasi cha $100 milioni ambazo watazitoa kwa watu (creators) mbalimbali ambao wanapandisha picha mnato ambazo zimetokea kuwavutia wengi. Pesa hizo zitaanza kutolewa kwa wote watakaokuwa wamekidhi vigezo kuanzia miezi michache ijayo mpaka mwaka 2022.

YouTube Shorts

Si aliyechapisha picha jongefu husika ndio anayeamua chapisho liwe liwekwe ndani ya kipengele husika bali ni wahusika wenyewe ndio wanaochambua na kuziweka kwenye kipengele husika kulingana na vigezo walivyoviweka.

TikTok mwezi Julai walitoa motisha ya namna hiyo mwaka jana mwezi Julai na baada ya muda kidogo wakaongeza dau kufikia $1 bilioni. Haya sasa kazi kwetu wale ambao tunapenda kupakia picha za mnato fupifupi.

Swali la kujiulia ni je, kipengele hicho kinapatikana duniani kote? Jibu ni hapana, kwa sasa kinapatikna kwa watumiaaji simu za Android nchini India pekee.

Vyanzo: TechCrunch, Gadgets 360

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania