Kipenyo (diameter) cha injini hii ni urefu wa mita nne (futi 13), injini iliyo kwenye hatua za majaribio inayotengenezwa na kampuni ya General Electric huko Marekani imepata sifa ya kuwa injini kubwa ya ndege za kibiashara kuwahi kutengenezwa.
Injini hiyo iliwashwa kwa mara ya kwanza wiki kadhaa nyuma katika kituo kiitwachwo GE Aviation’s Peebles Test Operation huko Ohio-Marekani na kufanyiwa majaribio.
Kulingana na GE, katika mahabara ya majaribio uundwaji wa injini ya ndege aina ya GE9X itawezesha ukusanyaji wa taarifa za injini na uwezo wake katika kuifanya ndege iweze kufanya kazi, kupata uthibitisho wa kimekanika na uhakiki wa kiasi cha joto ambacho injini hiyo kitapata pale inapotumika. Kwa kifupi ni injini janja, injini itakayoweza yenyewe kutoa taarifa zote muhimu kuhusu hali yake.
Feni ya mbele yenye urefu wa futi 11 (3.35m), injini hiyo inashikilia rekodi kwa kuwana uwezo wa nguvu ya kusukuma ndege kwa mpangilio wa 100,000lb. Hivi karibuni injini hiyo iliongezewa tenki kubwa zaidi kwa ajili ya kuhifadhi hewa na matenki ya mafuta ya ziada kwa ajili ya injini hiyo kubwa.
Inasemekana vipande vingi vya injini hiyo vimetengenezwa kupitia utumiaji wa teknolojia ya ‘3D printing’. Ingawa injini hii inanguvu sana kulinganisha na injini zilizopo sasa hivi bado injini hii inatumia mafuta kiasi kidogo huku ikiwa na uwezo wa kubeba ndege kubwa zaidi.
Injini hii iliyopiwa jina la GE9X pia ndio injini iliyo na kelele ndogo zaidi ukilinganisha na zinazotumika sasa hivi.
Teknolojia mpya katika ujenzi wa ndege zinachukua miaka mingi sana kukamilika. Inasemekana injini hiyo itapitia majaribio ya hali ngumu – kufanya kazi ikimwagiwa barafu, maji, vitu kama kuku n.k, mambo ambayo injini za ndege hukutana nayo mara kwa mara.
Injini hii inategemewa kutumika katika ndege mpya kubwa za familia ya Boeing 777x.
Chanzo: geaviation.com