Katika ulimwengu wa sasa vifaa vya kidijiti vinatengezwa kuweza kufanya kazi mbalimbali ambazo hata bila ya mhusika kutumia nguvu; teknolojia ya leo unaweza ukaiweka simu kwamba ikifika saa fulani izime/iwake, ipige kengele, intaneti izime, n.k.
Binafsi ni mtu ambaye natumia muda mwingi tuu kwenye mtandao nikifanya vitu mbalimbali na nimekuwa nikiwaza sana namna ambayo mtu anaweza kuamua saa ngapi intaneti izime kama ambavyo anaweza kupanga simu yake imkumbushe kuwa muda umefikia wa kufanya jambo fulani.
FIkiria wewe ni mmoja wa wale ambao wanapenda kufanya kazi mtandaoni usiku wa manane lakini ikafika muda fulani ghafla tuu ukapitiwa na usingizi huku ukiwa umeacha intanei ya kwenye simu yako inaendelea kutumika. Au umejiunga na kifuruushi cha usiku tu (intaneti) halafu inafika saa 12 asubuhi wewe umeshalala maana yake ni kwamba intaneti itanedelea kutumika mpaka hapo utakapoizima/kitakapokwisha.
Katika kutafuta suluhisho la suala hilo nikapata kuijua programu tumishi iitwayo CleverConnectivity +++Battery ambayo inapatikana Playstore. Je, nini kazi ya CleverConnectivity +++Battery?
>Kuzima/kuwasha intaneti (WiFi/3G). CleverConnectivity +++Battery inawezesha kuzima intaneti kulingana na vigezo ambavyo utakuwa umevichagua mathalani wakati wa kupumzika, pale ambapo intaneti haitumiki baada ya muda fulani kupita au ikifika muda fulani basi intaneti izime.
CleverConnectivity +++Battery inawezesha kuzima intaneti kulingana na vigezo mbalimbali ambavyo vimewekwa ndani ya programu tumishi husika.Ukitumia CleverConnectivity +++Battery inawezekana kuamua WiFi ijizime baada ya muda gani.
Ni matumaini yetu kuwa sasa kifurushi chako cha intaneti utakuwa na uwezo wa kukitumia ipasavyo kwa muda ambao utapendelea mwenyewe na tukumbuke kuwa CleverConnectivity +++Batteryinapatikana kwenye Android TU.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.
Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|
No Comment! Be the first one.