fbpx
Apple, IPhone, simu, Teknolojia

iPhone za mwaka 2019 zitakuaje? #Fununu

iphone-za-mwaka-2019-zitakuaje
Sambaza

Ni mwaka mwingine na tayari Apple walishaweka wazi kuwa mwaka huu wa 2019 tutarajie simu tatu kutoka kwao lakini swali linabaki kuwa simu hizo zitakuaje?

Kulingana na vyanzo mbalimbali vya taarifa tayari imeshabainika kwa mwaka huu Apple wamejipangaje kwenye ulingo wa ushindani wa bidhaa zikiwa zinakuja baada ya zile zilizototoka mwaka jana (2018); iPhone XS na XS Max.

>Muonekano

Simu za iPhone amabazo zitatoka mwaka huu zitafanana kwa kiasi kikubwa kimuonekano kama zile zilizotoka mwaka 2018. Hizi za mwaka huu zitakuwa na utofauti wa aina yake kwani inaelezwa kuwa Apple watatumia teknolojia ya USB Type C kwenye simu hizo.

INAYOHUSIANA  Alphabet yapeleka WiFi Puerto Rico kwa mfumo wa maputo yanayopaa

>Kamera

Apple wameona sio vibaya na wao wakafanya simu zao ziwe na ile idadi ambayo simu janja za nyingi za karibuni zinavyokuwa; hapa namaanisha kuwa na kamera tatu upande wa nyuma. Kamera hiyo ya tatu itakuwa na uwezo wa kuchukua eneo pana zaidi iwe picha/picha mnato, lakini pia kuwa na uwezo wa kurekebisha picha/video ili iweze kuonenea kwenye kioo na kuonekana vyema.

INAYOHUSIANA  Mapendekezo ya Apple kuhusu kuja na emoji zinazohusu walemavu
iPhone za mwaka 2019
iPhone za mwaka 2019: Toleo linalokuja la iPhone linaelezwa kuwa na kamera 3 upande wa nyuma.

>Mengineyo

Simu hizo zinategemewa kuwa na kipuri mama chenye kasi zaidi, teknolojia ya Face ID iliyo bora zaidi lakini pia kuongeza muda wa kupiga picha mubashara kutoka sekunde 3 hadi 6 kwenye kipengele cha Live Photos.

Kwa mipango ya mwaka 2020 Apple wanataka kuweka kamera ya 3D upande wa nyuma kwa simu zitakazotoka mwakani huku kamera hiyo ikiwa na uwezo a kuchukua picha/video katika madhari ya 3D.

Hizo ndio simu za Apple zikiwa na sifa ambazo zimeelezwa hapo juu. Kumbuka hizi ni fununu tuu kutoka vyanzo mbalimbali vinavyofuatilia kwa karibu utengenezaji wa vipuri vya simu vya makampuni mbalimbali. Mengi zaidi yataendelea kufahamika mpaka hapo watakapozindua bidhaa zao mwezi Septemba kama kawaida yao.

Vyanzo: The Verge, Bloomberg

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: , ,

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|