fbpx

Teknolojia ni mwiba kwa mawakala wa utalii

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Wakati dunia ikifurahia ukuaji wa teknolojia kurahisisha mambo mengi lakini kwa upande mwingine imekuwa pigo na kilio kwa watu na hilo limewakumba mawakala katika sekta ya utalii kwa kupoteza kipato kutokana na ujio wa teknolojia.

Mawakala wa utalii nchini Kenya wanapoteza hadi asilimia 60 ya soko kutokana na kuwa watalii sasa wanajihifadhia nafasi katika maeneo wanayotaka kutalii kwa njia ya mitandao na simu.

Tafsiri yake ni shilingi za Kenya takribani 39 milioni kila mwaka hazipatikani kutokana na uwepo wa teknolojia. Kwa sasa, watumiaji wa intaneti nchini humo ni milioni 36.09 kulingana na mamlaka ya mawasiliano nchini Kenya.

mawakala wa utalii

Kulingana na Chama cha wakala wa Usafiri (KATA) wamepoteza asilimia kubwa ya soko katika muda wa miaka 10 iliyopita.

Wakenya wengi wanapata habari kuhusiana na sekta hiyo kupitia tovuti hivyo kutohitaji tena mawakala kuwahifadhia nafasi kwenye hoteli au hata ndege. Mawakala hao sasa wameachiwa watu wanaosafiri kufanya biashara.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Utoaji wa talaka kwa njia ya simu wakemewa
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.