fbpx

Apple, IPad, IPhone, simu, Teknolojia

Apple yaendelea kuzikumbuka iPhone 5s, 6, 6 Plus na iPad

apple-yaendelea-kuzikumbuka-iphone-5s-6-6-plus-na-ipad

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Sambaza

Ni miaka kadhaa imepita tangu Apple watoe iPhone 5s, 6, 6 Plus na hata iPad toleo la nyuma zaidi lakini kampuni hiyo imeendelea kuwakumbuka wateja wake wanatumia vifaa hivyo vya kidijiti.

Tumia kila leo vifaa vyetu vya kiganjani lakini mara nyingi tunapuuza kufanya jambo muhimu sana kwa usalama wa wetu huko mtandaoni wakati tunaperuzi. Ndio, ni watu wachache ambao wana tabia ya kupakua masasisho mara yanapotolewa na wahusika na hicho si kitu kizuri.

SOMA PIA  Bitcoin yapata pigo baada ya wadau wake kutofautiana.

Kuna wakati unaweza ukawa unasubiri masasisho (hasa kama unatumia simu janja toleo la muda kidogo) mpaka ukafikri mpango huo wa kuendelea kupokea masasisho ya kiusalama kwa ajili ya kifaa chako cha kiganjani yamesitishwa lakini ni jambo la kufurahia kwani yeyote mwenye iPhone 5s, 6, 6 Plus na hata iPad toleo la miaka kadhaa (iPad mini 2), iPod touch/touch 6 wanaweza kupakua iOS 12.4.6.

Kimsingi sasisho hilo linalenga kurekebisha shida ndogondogo ndani ya kifaa husika, ufanisi na kuzidi kujidhatiti kwenye suala zima la ulinzi wa simu janja kutodukuliwa. Kuweza kulishusha unakwenda kwenye settings>>general>>software update na ikishafanikiwa kulipata bofya download & install.

iPhone 5s
iOS 12.4.6 lapelekwa kwenye iPhone 5s, 6, 6 Plus, iPad mini 2, iPod touch.

Kamwe usipuuze masasisho kama hayo kwenye Android ama iOS kwani wahusika wanayaleta kwa nia nzuri tuu ya kufanya simu janja yako iendelee kufanya kazi vizuri na isiweze kudukuliwa kirahisi.

Vyanzo: GSMArena, WCC Tech

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Sambaza

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|