Watu watatu wamefikishwa mahakama ya mwanzo ya Kinondoni kwa tuhuma za kuiba simu za Mamlaka ya Kudhibiti wa mawasiliano Tanzania (TCRA).
Washtakiwa hao ambao ni mlinzi wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania, BW. Rashid Abdallah, Bi. Fatuma Rajabu na Bw. Idd Bago wanatuhumiwa kuiba simu za TCRA huku wakijua ni kosa kisheria. Abdallah ndiye aliyeiba simu zote na kuwapa wenzake kuziuza.
Mwendesha mashtaka aliwasomea watuhumiwa hao akidai Januari 9, 2018 saa 6 mchana katika ofisi za TCRA mlinzi Abdallah aliiba simu 17 aina ya KZG, simu nyingine sita (6) ambazo ni Dougeex51, Tecno HSL, Samsung Galaxy T5 Prime 1Â na KZG min 1 ambapo mwendesha mashtaka huyo alisema simu hizo zina jumla ya thamani yake ni shilingi 4,570,000.
Washtakiwa hao kwa mara ya kwanza walifikishwa mahakamani Septemba 17, 2018 na kusomewa mashtaka hayo ambapo washtakiwa Abdallah na Fatuma walikana mashtaka hayo lakini Idd Bago alikubali kosa.
Aidha kesi yao ilitajwa tena Septemba 23 lakini imeahirishwa mpaka Oktoba, 1 2018 baada ya mshauri wa mmoja wa mahakama kutokuwepo mahakamani hapo.