Bado hakuna taarifa rasmi ya kutoka toleo la karibuni lakini inaonekana kwamba WhatsApp inatarajia kuanzisha muonekano wa giza (Dark Theme) katika programu yake hiyo pendwa.
Kwa mujibu wa tovuti ya WABetaInfo wamebainisha hilo kwamba lipo njiani kuanza kupatikana kwa watumiaji wa WhatsApp. Kuja kwa kitu hicho itakuwa ni habari njema kwa watumiaji wa WhatsApp iliyo rasmi ambapo watakuwa na uhuru wa kubadilisha muonekano wa WhatsApp kwa namna watakavyovutiwa.