fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Android apps Intaneti iOS Mtandao wa Kijamii simu Teknolojia whatsapp

Muda wa jumla kwa watumiaji wa WhatsApp

Muda wa jumla kwa watumiaji wa WhatsApp

Spread the love

Kwa mujibu wa ripoti mpya watumiaji wa WhatsApp duniani kote tukiangazia muda wa jumla inaelezwa walitumia saa bilioni 85 kwenye programu hiyo katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.

Ripoti hiyo ambayo imeenda mbali zaidi na kubainisha kuwa kila mtu anatumiwa wastani wa saa 11. 425 na takwimu zinaonyesha WhatsApp ina watumiaji karibu bilioni 1.5.

Muda wa jumla

Saa 30 bilioni zimetumia kuperuzi mtandao wa kijamii wa Facebook.

WeChat imeshika nafasi ya pili kwa kutumiwa zaidi baaada ya WhatsApp. WeChat ni mtandao maarufu zaidi nchini Uchina unaotumika kwa mawasiliano badala ya WhatsApp ambayo hairuhusiwi nchini humo.

Kwa upande michezo (Games) iliyochukua saa nyingi kuchezwa ni My Talking Tom, Candy Crush Saga, Fortnite, Lords Mobile, Subway Surfers, Helix Jump, Slither.io, PUBG Mobile na Fishdom.

Michezo hiyo kwa jumla ilitumia saa bilioni 3.83 kujifurahisha kupitia watumiaji wa simu duniani.

Muda wa jumla

Ripoti ya utafiti inaonyesha watu wa Marekani wanatumia angalau saa tatu na nusu kwa siku kutumia simu.

Progamu 10 ambazo zinatumiwa zaidi ni WhatsApp, WeChat, Facebook, Messenger, Pandora, YouTube, Instagram, Twitter, Google Maps, na Spotify.

SOMA PIA  Robohon: Roboti ambaye pia ni simu janja
Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania