fbpx

Duo yapelekwa kwenye tabiti na iPad

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Wakati programu tumishi, Google Duo inatoka iliifanya Google kuingia kwenye ramani ya ushindani na Skype, Messenger, Facetime lakini sasa wameamua kupanua wigo wa upatikanaji wake kwa kuwekwa kwenye tabiti na iPad.

Baada ya kuwepo kwenye simu za Android na kutokuwa na masasisho makubwa Google wameona ni wakati wa kutanua mipaka na kuwafikia wale ambao wanatumia iPad/tabiti.

Je, Google Duo ni nini?

Kwa muhtasari tu ni programu tumishi ambayo inawezesha mawasiliano kwa njia ya picha jongefu/maandishi; kama ilivyo kwenye WhatsApp, Viber, n.k.

Awali, Google Duo iliundwa na kufanya kazi vyema kwenye intaneti hafifu na hivyo kufanya mawasiliano kutokuwa ya tabu kutokana na ilivyotengenezwa kufanya kazi.

tabiti na iPad

Google Duo-Programu tumishi inayoweza kufanya mawasiliano kwa njia ya picha mnato/maandishi.

Wakati programu hiyo inatoka haikuwa na ushawishi mkubwa lakini kadri siku zilivyosogea ikaonekana kuvutia watu kutokana masasisho mbalimbali hasa kwa wanaotumia tabiti zenye kioo kipana.

tabiti na iPad

Kama ni mawasiliano kwa njia ya mnato itakuwa ni rahisi watu wote kuonekana kwenye kamera.

Hivi sasa Google Duo inapatikana kwenye iPad na tabiti sasa ushindwe wewe tuu kuipakua na kuwa nayo kwenye kifaa chako.

Vyanzo: Engadget, The Verge

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Sony Xperia 1: Simu yenye upekee wa aina yake
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.