Katika mkutano/maonyesho wa IFA 2018 ambayo yamefanyika Berlin, Ujerumani BlackBerry wametua vyema mkutano huo kwa kutambulisha pacha wa BlackBerry Key 2.
Pacha anyezungumziwa kwenye makala hii ni BlackBerry Key 2 LE aliyetambulishwa kwenye maonyesho ya IFA 2018 huko Ujerumani. Simu hiyo inauzwa bei rahisi kuliko mtangulizi wake, kicharazio ambacho ni rahisi kubonyeza na rangi mbalimbali tofauti na toleo lililopita.
Sifa/Undani wa BlackBerry Key 2 LE ni kama ifuatavyo:-
Kipuri mama/Kioo. BlackBerry Key 2 LE inatumia Snapdragon 636 processor na urefu wa kioo ukiwa inchi 4.5.
RAM/Memori ya ndani. Simu hiyo ina RAM ya GB 4 na diski uhifadhi ni aidha GB 32 au GB 64. Pia ina sehemu ya kuweka memori ya ziada.
Kamera.Masuala ya picha hapo kuna kamera 3 kwa ujumla wake; zile za nyuma zina MP 13 na MP 5 bila kusahau nakshi ya mwanga (flash). Kamera ya mbele ina MP 8.
Betri/Programu endeshi. BlackBerry Key 2 LE ina betri yenye 3000mAh. Pamoja na hilo simu hiyo ina teknoljia ya kuchaji kifaa hicho haraka. Programu endeshi ni Android kama kawaida.
Usalama. Kwa mara nyingine BlackBerry imeendelea kutumia DTEK hii ikiwa ni programu wezeshi ambayo inaongeza ulinzi kwenye simu hiyo lakini pia kuweza kuingia kwenye soko la programu tumishi ni lazima uweke alama ya kidole ndio mengineyo yafuate.
Bei yake imekuwa ni kivutio kikubwa ukilinganisha na mtangulizi wake; BlackBerry Key 2 LE ya GB 32 ni $399|Tsh. 917,700 na $499|Tsh. 1,147,700 kwa yenye GB 64.
Vyanzo: CNET, The Verge, Android Central.