Simu janja za Samsung huwa zina ‘Menu’ maalamu ya majaribu au kwa lugha nyingine tunaweza tunaweza tukasema ni ile ‘Menu’ ya uhakiki.
Wachache sana ndio wanajua jambo hili na wengine wanachanganya na kuusema ‘Menu’ hii ndio itakayoweza kumhakikishia mtu kama simu yake ya Samsung Gallaxy ni feki au orijino. Jambo hili sio la kweli kwani kuna hata kwa baadhi ya simu feki za Samsung ‘Menu’ hii ilikua inafanya kazi kama kawaida.

Pengine swali kubwa ambalo unaweza ukajiuliza sasa ni jinsi gani ambavyo unaweza ukatumia kuipata ‘Menu’ hii. Ni rahisi sana kwani utaweza kuipata kwa kuandika baadhi ya tarakimu katika simu yako.
Kama unatumia simu ya Samsung Galaxy nenda katika uwanya wa kuandika namba (kama ukitaka kupiga namba) na kisha weka tarakimu hizi *#0*#. Ukishamaliza andika hizo tarakimu kuna ‘Menu’ itajitokeza.

‘Menu’ hii ikitokea unaweza ukahakikisha mambo yafuatayo:-
– Kuhakiki baadhi ya rangi katika simu
– Kuhakiki Uwezo wa mngurumo (vibration)
– Kuhakiki uwezo wa Sensa
– Kuhakiki uwezo wa tachi (Touch)
– Kuhakiki uwezo wa spika na mengine mengi
‘Menu’ hii ina umuhimu mkubwa sana hebu fikiria kama unahisi simu yako ya Samsung Galaxy katika kioo chake unahisi kuna maeneo ambayo unahisi touch yake inasumbua. Unaweza ukatumia ‘Menu’ hii kuhakikisha hilo