Programu endeshi ni kiungo muhimu sana katika kuwezesha mawasiliano kati ya mtu na simu janja na mpaka sasa kuna toleo mbalimbali ambapo kwa upande wa Android zimefika 12 hadi sasa.
Septemba 3 2019, itabaki kwenye kumbukumbu kwani ndio tarehe ambayo Android 10 ilitoka na hadi leo ni kinara kwa kutumika kwenye rununu nyingi. Ingawa ina zaidi ya miaka miwili tangu itoke lakini bado inaonekana kuwepo kwente simu jaja nyingi zinazotumia Android.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotelewa hivi karibuni zinaonyesha Android 10 ndio nambari moja ikiwa na 26.5% ya simu janja huku Android 11 ikifuata nyuma yake kwa 24.2% ya rununu za Android ndio zinatumia Android 11. Baada ya hao 18.2% zinakwenda kwenye Android 9 Pie, 13.7% ni Oreo, Android 7 & 7.1 Nougat-6.3%, Android 6 Marshmallow ni 5.1%. Karibu 3.9% bado wapo kwenye Android 5 Lollipop, 1.4%-Android 4.4 KitKat na toleo la zamani kabisa (Android 4.1) inatumika kwenye 0.6% ya vifaa vyote vya Android.
Mchoro unaonyesha mgawanyo wa vifaa vya Android ambavyo vinatumia toleo mbalimbali za programu endeshi (Android).
Kwa upande wa Android 12 takwimu zake bado hazijajulikana na ukizingatia ndio toleo jipya kabisa ambalo bado halijafika kwenye simu janja nyingi na takwimu hizi zinatokana na wanaoingia Playstore katika kipindi cha siku saba za wiki.
Je, wewe msomaji wetu simu yako inatumia Android 10 ama toleo la nyuma/mbele zaidi? TeknoKona tupo hapa kila siku hivyo tunapenda kupata maoni yenu na daima usisite kutembelea tovuti yetu ili kuweza kuhabarika lakini pia kujifunza.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
No Comment! Be the first one.