fbpx
Kompyuta, Microsoft, Teknolojia, Uchambuzi

Microsoft Surface Studio: Microsoft kushindana moja kwa moja na kompyuta za iMac

microsoft-surface-studio-microsoft-kushindana-moja-kwa-moja-na-kompyuta-za-imac
Sambaza

Microsoft watambulisha rasmi kompyuta yao ya kwanza ya desktop, inafahamika kwa jina la Microsoft Surface Studio na ina sifa nzuri sana na inalenga kutumika sehemu ambazo kompyuta za Mac tayari zinafanya vizuri.

Microsoft wametambulisha kompyuta hiyo jijini New York na hii ni baada ya tetesi za muda mrefu.
Muonekano wa Microsoft Surface Studio.
Microsoft Surface Studio
Muonekano wake
Muonekano wa kompyuta ya Surface Studio
iMac ni kompyuta za mezani (desktop) kutoka Apple zinazotumiwa sana na watu wanaoitaji kompyuta za uwezo wa juu kama vile wabunifu n.k, na kompyuta hii kutoka kwa Microsoft inalenga kuizidi ubora hadi iMac na kwa kiasi kikubwa tunaweza sema wamefanya cha kitofauti sana.
Kama vile kwa iMac, Microsoft Surface Studio imeunganisha vitu vyote muhimu vya kompyuta katika umbo moja.

Sifa za Microsoft Surface Studio

Kuna matoleo ya aina mbili, kulingana na prosesa zilizotumika. Kuna toleo la Intel Core i5 na Core i7.
.
> Ya Intel Core i5
  • RAM GB 8
  • Kadi ya GPU ya Nvidia 980 2GB
  • Uhifadhi wa TB 1
  • Bei $3,000 (Zaidi ya Tsh 6,000,000/=)
> Ya Intel Core i7
  • RAM GB 32
  • Kadi ya GPU ya Nvidia 980 4GB
  • Uhifadhi wa TB 2
  • Bei $4,200 (Zaidi ya Tsh 8,400,000/=)
Spika za kiundani, port nne za USB 3.0, eneo la memori kadi pamoja na intaneti.
Kipande cha display/kioo cha kompyuta hii ya Surface kinaweza kupinda na kulala hadi kufikia nyuzi 20, hii inarahisisha utumiaji wa kompyuta kwa kazi kama vile uchoraji, ubunifu mbalimbali na uandikaji document. Kwa kompyuta hii utaweza tumia teknolojia mguso (touch) au keyboard.
Muonekano wa Surface Studio ikiwa imelazwa nyuzi 20.
Muonekano wa Surface Studio ikiwa imelazwa nyuzi 20.
Display yake ina ukubwa wa inchi 28 na ina jumla ya pixels milioni 13.5…hii ni kiasi kikubwa sana. Hii itasaidia kiwango cha ubora wa picha na rangi. Ni kiwango cha juu sana.
Pia wametambulisha kidude kidogo kilichokuja na jina la Surface Dial – kifaa hichi ambacho kitapatikana kwa dola 100 za Marekani, takribani Tsh 200,000/=.
Microsoft Surface Dial
Jinsi kidude cha Surface Dial kinatumika
Kutumia Surface Dial chenye teknolojia za kimguso mtu ataweza kufanya mambo mbalimbali ambayo mwanzoni yaliitaji msaada wa kutumia Kipanya na kuchukua hatua mbalimbali ili kukamilisha mambo… Mfano kuzungusha au kusogeza kitu n.k. Angalia hapa chini utumiaji wa teknolojia hii
Surface Dial vitaanza kupatikana Novemba 10 na vitaweza kutumika ata kwenye Surface Book na Surface Pro.
Kompyuta za Surface Studio zitaanza kupatikana mwezi wa 12 tarehe 15.

Vipi unamtazamo gani juu ya kompyuta hii?

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTube, Telegram na Google Plus

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Utaweza ku'upgrade' Kwenda Windows 8 Kwa Dola 39.99
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |