fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Nokia simu Teknolojia Uchambuzi

Uchambuzi wa Nokia C2, uwezo na sifa.

Uchambuzi wa Nokia C2, uwezo na sifa.

Kampuni ya Nokia yenye makao makuu yake nchini Finland kwa wakati huu inatoa simu ambazo zinatumia mfumo endeshi wa Android. Hii ni baada ya kampuni hio kuachana na mfumo endeshi wa Windows.

Nokia C2 ni moja ya simu zao katika bei ya chini zenye ubora mzuri na thamani kwa gharama yake. Kutokana na ukuaji wa teknolojia siku hizi soko la simu janja lipo juu na hii ni kutokana na mengi ambayo bidhaa hizo zinaweza kufanikisha mahali popote ambapo mtu anaweza kuwepo bila kusahau kufanikisha mawasiliano kwa urahisi, uharaka wa aina yake.
Sifa za simu hii ni:

  • Kioo (Display) cha teknolojia ya LCD chenye ukubwa wa inch 5.7,
  • Mfumo endeshi wa Android 9.0 (Go Edition),
  • RAM ya GB 1 na diski uhifadhi ya GB 16,
  • Kamera ya megapixel 5 nyuma na kamera ya megapixel 5 mbele,
  • Betri yenye uwezo wa 2800 mAh, 
  • Simu hii inasapoti teknolojia ya mawasiliano ya 4G, pia teknolojia ya Bluetooth na WiFi pamoja na huduma ya redio, bei yake ni zaidi ya Tsh. 165,600.Nokia C2
SOMA PIA  Apple Na Samsung Watupwa Mbali: Huawei Imeongoza Mauzo China Katika Robo Ya Pili Ya 2016!

Pia, Nokia C2 ina sehemu ya kuchomeka waya wa earphones, sehemu ya kuchomeka waya wa chaji aina ya micro USB 2.0. Haina teknolojia ya utambuzi wa alama za vidole na huja katika matoleo mawili ya rangi- Samawati na Nyeusi.

Chanzo: GSMArena

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania