Tulishaandika kuhusu taarifa iliyokuwa bado haijatoka rasmi ya kwamba kampuni ya Apple inajiingiza katika utengenezaji wa magari, na sasa suala hili halina ubishi tena. Google tayari wamefika mbali kabisa katika teknolojia ya utengenezaji wa magari yanayojiendesha yenyewe na sasa Apple pia wamejitupa katika teknolojia hiyo hiyo.
Soma – iPhone hadi iCar: Je Apple watatengeneza Gari?
Uhakika mkubwa juu ya kampuni ya Apple kujiingiza kwenye suala la utengenezaji wa magari umejulikana baada ya injinia mmoja wa kampuni huyo kwenda kuomba kibali cha kutumia uwanja mmoja wenye barabara kadhaa nchini Marekani kwa ajili ya majaribio ya magari hayo.
Kampuni ya Google (kwa sasa ALPHABET) tayari imefika mbali zaidi katika teknolojia ya magari yanayojiendesha yenyewe na inaonekana Apple pia imeamua kutoachwa nyuma katika hili. Wengi wanaona teknolojia ya namna hii (magari ya kujiendesha yenyewe) itakuwa kubwa sana miaka michache baadae. Na kikubwa zaidi wote, Google na Apple, wanaamini kuna umuhimu mkubwa wa vifaa kama simu na tableti kuweza kuwasiliana moja kwa moja na gari lako. Fikiria uingie kwenye gari na uweze kutumia huduma mbali mbali za simu yako bila kushika simu hiyo.
No Comment! Be the first one.