Simu zetu za sasa, yaani simu janja ni simu zilizofanikiwa kubeba teknolojia mbalimbali za kipekee ndani yake zaidi ya kupiga na kupokea simu tuu, au na kusms kama ilivyokuwa zamani. Simu za sasa zinauwezo kubeba sifa ya vifaa vingine vingi kama vile kompyuta, kamera n.k
Leo tunakuletea apps tunazozichukulia kama apps bora zaidi katika masuala ya mafaili mchapisho (Documents) na nyingine zinazohusiana na masuala kama hayo.
CamScanner
Hii ni app ambayo inakusaidia kuweza kuskani documents zako kwa kutumia kamera yako. Iwe ni document ya maneno tupu au picha app hii itaweza kukufanyia hayo yote. Inauwezo wa kutengeneza kurasa zaidi ya moja kuwa sehemu ya faili moja na kuhifadhi (save) katika mifumo ya PDF na mingine mingi.
Google Play -> CamScanner | App Store (Apple)
Word Lens
Fikiria uwezo wa kutafsiri maneno yaliyo kwenye karatasi/document yeyote kwa kutumia kamera yako ya simu, app ya Word Lens inakuwezesha kufanya hilo. Kwa kutumia app hii utaweza kutafsiri maandishi ya lugha mbalimbali yawe yameandikwa kwenye gazeti, bango la barabarani n.k, unachoitaji ni simu/tableti yenye kamera tuu.
Google Play ->Word Lens
CamCard
Fikiria kama jambo hili lingewezekana…. Umepewa kadi ya mawasiliano (business card) na mtu, na ungependa kuwa na taarifa zote kutoka kadi hiyo kwenye simu yako badala ya kubeba beba makadi kibao….hili linawezekana na ndio kitu kinachofanywa na app ya CamCard. Kutumia app hii, unaweza kupiga picha kadi ya mawasiliano ya mtu na app hii itasoma na kurekodi taarifa zote kutoka kadi hiyo kwenye orodha yako ya taarifa za mawasiliano, yaani ‘Contacts’ zako. Na taarifa ambazo CamCard itazichukua kutoka kwenye ‘business card’ ni pamoja na jina la mtu, namba ya simu, barua pepe na mengineyo.
CamCard Google Play | App Store (Apple)
Dropbox
Tushawahi andika kwa undani kuhusu Dropbox (Soma – ). Hii ni huduma inayotumia teknolojia ya Cloud kukuwezesha kupata mafaili yako tena ata pale ambapo kifaa chako kikipotea au kuharibika. Ukipakua app hii katika simu yako na kufungua akaunti basi utaweza kuchagua mafaili mbalimbali ambayo yatakuwa yanahifadhiwa kupitia mfumo wa DropBox. DropBox itahakikisha inakuhifadhia mafaili hayo kwenye akaunti yako mtandaoni na hivyo kama utapakua app hii kwenye kifaa kingine utaweza kuyapata mafaili hayo yote. Pia unaweza ukaingia tuu kwenye mtandao wao wa DropBox.com na kuangalia mafaili yako yote.
DropBox – Google Play | App Store (iTunes)
Google Drive
Kama vile app ya DropBox, Google Drive inatumia teknolojia ya Cloud kukuwezesha kuhifadhi mafaili yako katika mfumo wa ‘Back up’, yaani utaweza kuyapata kwenye mtandao wa Google Drive ata pale unapoteza kifaa hicho. Karibia kila kinachoweza kufanyika na DropBox kinawezekana kwenye Google Drive pia. Na kama tayari una akaunti ya Google basi ata uhitaji kutengeneza akaunti mpya. Uwezo mwingine wa zaidi kwa Google Drive ni pamoja na uwezo wa kuandika na kufanyia mabadiliko mafaili yako ya kwenye mfumo wa ‘word document’ na excel.
Google Drive – Google Play | App Store (iTunes)
Apps kutoka Microsoft
Hapa naongelea Microsoft Word, Microsoft Excel na Microsoft PowerPoint. Apps zote hizi zinapatikana bure kabisa katika simu na tableti za jamii ya Android na iOS. Apps hizi zinapatikana bure na zinakuwezesha kufungua, kusoma na kuandika document zako kwa urahisi zaidi kwenye simu au tableti yako.
Google Play | Excel | Word | PowerPoint
App Store | Excel | Word | PowerPoint
No Comment! Be the first one.