fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Teknolojia

Emirates Watangaza Safari Ndefu Zaidi Ya Ndege Duniani!

Emirates Watangaza Safari Ndefu Zaidi Ya Ndege Duniani!

Spread the love

Emirates itakua ikishikilia mikoba ya kuwa ndege yenye safari yenye ruti ndefu zaidi duniani kutokana na huduma yake ya safari kutoka Dubai mpaka jiji la Panama. Safari hii itakua ni ya moja kwa moja. Huduma hii inategemewa kuanzishwa rasmi mwezi januari

Safari hiyo itakuwa na urefu wa kilomita 13,821 ambazo ni maili 8,590 ambazo pia ni kilomita 17 (maili 10.56) zaidi ya ile ambayo itakua ruti ndefu  ya ndege katika nafasi ya pili. Ruti ya safari hiyo ni kutoka Sydney mpaka Dallas kwa kutumia ndege za Qantas.

SOMA PIA  Mambo 16 Ya Ukweli na ya Kuvutia Kuhusu Bill Gates!

Kwa Ruti hizo za anga Emirates itatumia ndege ya Boeing 777-200LR, ambayo pia safari yake itachukua takribani masaa 17 na dakika 35, Kampuni hiyo ya ndege (Emirates) ilisema

Emirates Airlines At Dubai Airport

Shirika La Ndege La Emirates Katika Uwanja Wa Ndege Wa Dubai

Pia ruti hiyo ya dubai mpaka jijini panama haitaweka rekodi kwa sababu kulikua na ruti defu zaidi ya ndege iliyokua ikimilikiwa na Singapore (Singapore Airlines). Ndege ilikua ikichukua abiria kutoka Singapore na Newark, New Jersey takribani kwa zaidi ya umbali wa kilomita 15,344 ambazo ni maili 9534.32 na ilikua ikichukua masaa 19 tuu.

SOMA PIA  Stratolaunch: Ndege kubwa zaidi duniani yapaishwa nchini Marekani

Sasa jiji la Panama litakua ndio geti la wageni (Wanaotumia ndege ya Emirates) kuingi Amerika ya kati, Kaskazini kusini na hata pande zingine. Kutoka kwa mwenyekiti wa ndege hizo (Emirates) amesema kuwa pia ruti hiyo itasaidia katika uwezo wa bidhaa zinazoingia kutoka njee ya nchi kama vile elektroniki, bidhaa za mashine na hata madawa (ya matibabu)

Ndege ya Boeing 777-200LR kwa ruti hiyo itakua na siti 266 kwa jumla. Mpaka sasa Emirates ruti yao kubwa ni kutoka Dubai mpaka Los Angels ambayo ina  umbali wa kilomita 13,420 (maili 8338.8) na inatumia ndege aina ya Airbus A38- superjumbo.

SOMA PIA  Instagram Kuondoa Kipengele Cha Ramani (Maps) Katika App Yake!

Kama wewe ni mpandaji mzuri wa dege hii itakugusa. Kuna baadhi ya sehemu mtu ukitaka kwenda ni lazima uunganishe ndege — mfano mbinguni (hah!)– teknolojia inazidi kukuwa na pia iinarahisisha usafiri wa anga. Itafika kipindi hata safari yako iwe ya mbali kiasi gani utapanda ndege moja tuu. Ningependa kusikia kutoka kwako, tuambie mawazo yako

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania