fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Android Samsung simu Teknolojia

Tatizo la vipuri vya Qualcomm kwenye simu za Samsung

Tatizo la vipuri vya Qualcomm kwenye simu za Samsung

Spread the love

Siku kadhaa zilizopita tuliandika kuhusu vipuri mama vya Qualcomm kuwa na tatizo hivyo kuhatarisha usalama wa simu janja ambazo zinatumia kifaa lakini Samsung wametoa neno lao.

Moja ya makapuni makubwa ambayo yanatumia vipuri mama vya Qualcomm ni Samsung ambao kufuatia taarifa iliyohusisha kifaa hiyo wateja wa rununu za Galaxy kuna neno kwa ajili yao. Katika taarifa waliyoitoa Samsung hivi karibuni wamebaninisha tayari suala hilo wameshalishughulikia kwa baadhi ya simu janja ambazo zinatumia kipuri mama husika iwapo watakuwa wamepakua masasisho ya kiusalama yaliyotolewa Mei Mosi 2021 au yaliyotolewa baada ya tarehe hiyo.

Qualcomm

Taarifa inayohusisha baadhi ya simu janja za Samsung na tatizo la vipuri mama vya Qualcomm.

Najua utakuwa unajiuliza ni simu gani za Samsung ambazo tayri zipo salama kufuatia shida iliyoonekana kwenye vipuri mama tajwa. Jibu ni kwamba Samsung haijaweka wazi orodha ya rununu ambazo zimeshashughulikiwa kuhusiana na tatizo lililohusisha vipuri vya Qualcomm.

Ushauri wa bure ambao TeknoKona tunatoa ni kwamba kila mtu anayetumia simu janja za Samsung basi ashushe masasisho ya hivi karibuni ili kuweka kifaa chako salama na mwisho tuwe na tabia ya kushusha vitu vya aina hii.

Je, una tabia ya kushusha masasisho kila yanapotoka? Tunakaribisha maoni yako na usiache kutufuatilia kila leo kwa habari mbalimbali zinazohusu teknolojia.

Vyanzo: GSMArena, 9to5Google

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Comments

  1. […] usalama wa simu janja zake kwa kupeleka masasisho yanayolenga kuboresha, kurekebisa lakini pia kuimarisha usalama wa kifaa husika na safari hii rununu kutoka familia ya Galaxy S10 imepelekewa mambo […]

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania