fbpx
apps, Intaneti, Netflix

Netflix Kuwa Juu Zaidi Wakati Amazon Na Disney+ Wakifukuzia!

netflix-kukuwa-zaidi
Sambaza

Netflix ni mtandao unajihusisha na ku’stream tamthilia na filamu, kwa sasa ndio mtandao mkubwa ambao unajihusisha na mambo hayo. Ukiachana na kampuni ya Netflix, kuna kampuni zingine kama Amazon na Disney+ ambazo nazo zinakuja kwa kasi.

Netflix imetabiri wazi wazi kuwa mpaka mwaka huu kuisha inaweza ikawa imeshapata ‘Subscribers’ milioni 190. Kumbuka utabiri  huu umetokea pia baada ya janga la virusi vya corona kutawala dunia. Ni wazi kuwa watu wengi wamekua wakijiunga na huduma kama hizi wakiwa karantini/lockdown au hata wakiwa home ili mradi iwaepushe na uzururaji.

INAYOHUSIANA  Huduma ya Usafiri wa Uber Kuja Tanzania, Uganda na Ghana
Muonekano Wa Netflix
Muonekano Wa Netflix

Makampuni mengi yanakimbilia katika huduma hizi kwani kwa sasa ndio teknolojia inapohamia huku, na Netflix kwa bahati ni moja kati ya makampuni makongwe sana ambayo yalianza kufanya hivyo kitambo ukilinganisha na mengine ndio maana mafanikio wanayaona.

Kampuni kama Disney+ (kampuni mama Walt Disney Co) ni kampuni tishio sana kwani inakuja na vitu vingi ambavyo inaifanya kampuni hiyo kuwa tishio la baadae, kwa mfano kampuni hiyo ina hati miliki ya filamu nzuri sana za zamani.. ukiachana na hivyo kampuni ya Walt Disney inamiliki pia studio ya Pixar, na filamu zenye majina makubwa kama Marvel, na Star Wars.

INAYOHUSIANA  Wachoma moto minara ya 5G kwa hofu ya kwamba 5G inasambaza Coronavirus

Disney+

Muonekano Wa Disney+

Ishu nyingine kubwa ni kuwa na fasihi nzuri ambazo zitawalazimu watu kununua huduma yako, kwa mfano kampuni ya Netflix mpaka sasa imeweza kushinda mioyo ya wengi kwa kuwa na filamu na tamthilia nzuri ambazo wanazitengeneza wenyewe  na kuzionyesha wenyewe tuu.

Pia Netflix imewahi kuanza kupatikana katika mataifa mengi zaidi duniani wakati bado huduma hizo zingine zinaanza kusambaa taratibu. Kwa kuwahi kuanza pia Netflix imeweza kuwa na mapato makubwa na pia kuvutia uwekezaji mkubwa na kwa sasa kuipa uwezo wa kutengeneza filamu na tamthilia nyingi kila kukicha, tena kwenye mataifa mbalimbali. Huduma hizi zingine bado hazifikisha uwezo wa kufanya hivyo.

INAYOHUSIANA  Google Hangouts kufikia tamati ya kutumika

Kwa haya machache bado inaonekana Netflix wataendelea kuwa juu kwa kipindi kirefu.

Je wewe una mtazamo gani? Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika sehemu ya maoni, wewe ni nini maono yako kuhusiana na hili pia kumbuka kutembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKona kwa habari/makala kedekede zinazohusu teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Hashdough

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com