fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

apps Data TikTok

Serikali ya China inapinga ulazimishwaji wa TikTok kuuzwa

Spread the love

Mvutano baina ya China na Marekani kuhusu Tik Tok bado waendelea ambapo serikali ya China inasema ni bora ione TikTok inafungiwa nchini Marekani kuliko kuwafanya TikTok kuuzia kwa nguvu sehemu ya app hiyo kwa kampuni ya kimarekani.

Beijing imepinga uuzwaji wa kilazima wa sehemu ya app ya Tik Tok nchini Marekani. “Ni bora app hiyo ya video fupi ifungiwe kutumika nchini marekani” Watu wa tatu wenye ufahamu wa moja kwa moja wa suala hilo walisema hivyo siku ya ijumaa, Ripoti ya Reuters inataja.

Serikali ya China inapinga ulazimishwaji wa TikTok kuuzwa

Serikali ya China inapinga ulazimishwaji wa TikTok kuuzwa

ByteDance na mwanzilishi wake Zhang Yiming wameshikwa katika mapigano kati ya wakuu wawili wa ulimwengu. China inaona kama TikTok itauzwa basi serikali yao inaweza kuonekana haina nguvu, hasa hasa katika kutetea makampuni yake.

“Maafisa wa China wanaamini kuuzwa kwa nguvu kutafanya ByteDance na China kuonekana dhaifu juu ya shinikizo kutoka Washington”. ByteDance ndio kampuni mama inayomiliki TikTok. 

Pia inakuja siku chache kabla ya tarehe ya mwisho ya tarehe 15 Septemba ya Donald Trump kwa TikTok kupata nyumba mpya na kampuni ya Marekani.  Wataalam wamesema hakuna uwezekano wa mpango huo kutekelezeka haraka, lakini Trump alisema Alhamisi angeongeza tarehe ya mwisho.

ByteDance Kampuni ya china  inayomiliki programu hio ya Tik Tok imekua kwenye maongezi ya kibiashara na wanunuzi ambao ni kampuni za Marekani za Microsoft na Oracle juu ya kuwauzia sehemu ya app ya TikTok hasa ikiwa ikitoa jukumu la utunzaji data za watumiaji wa app ya TikTok kwa kampuni ya kimarekani. Rais wa Marekani Donald Trump ametishia kuifungia app hiyo nchini Marekani kama hakutakuwa na umiliki wa aina yeyote kutoka kwa kampuni ya nchini Marekani.

Rais Trump hana imani kabisa na usalama wa data za watumiaji wa app hii inayokua kwa kasi inayomilikiwa na kampuni kutoka China, huu ni muendelezo wa hatua zingine kali zilizochukuliwa dhidi ya Huawei.

Je! Kwa mtazamo wako unahisi China itakubali kuendelea kuona kampuni hii ikilazimishwa kutoa umiliki wa baadhi ya kazi zake kwa makampuni ya Marekani au wataingilia kati?

SOMA PIA  Google kusitisha uungwaji mkono wa app za Chrome kwa linux Mac na Windows

Endelea kutembelea kurasa zetu kujua hatma ya mzozo huu kati ya mataifa mawili yenye nguvu duniani kwa sasa – hasa kwenye nyanja za teknolojia?

Vyanzo: Engadget na vyanzo mbalimbali

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania