fbpx
apps, Gemu, Mtandao, Teknolojia

Pokemon Go: Gemu Tishio kwa mitandao ya kijamii

pokemon-go-tishio-kwa-mitandao-ya-kijamii

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

Kwa wamiliki wa hisa za mitandao kama Twitter Facebook, Snapchat na mitandao mingine ya kijamii basi bwawa limeingia ruba wikiendi hii  iliyopita baada ya gemu la Pokemon Go kuingia sokoni na kuchangamkiwa kwa kasi ya ajabu na watumiaji wa gemu hilo kwa nchi za Marekani New Zealand na Australia.

pokemon Go

Mpaka sasa Pokemon Go ina trend katika masoko ya app ya Google (Play store) na Apple (app store) katika nchi ambazo gemu hili limezinduliwa, lakini pia Pokemon imekuwa ni moja ya maneno yaliyotafutwa zaidi katika google.

INAYOHUSIANA  Badili Picha ya Kufungua Windows 7 iwe Utakavyo na Mengineyo

Takwimu zinaonesha mpaka sasa!

 • Gemu hili limewekwa katika simu nyingi za Android nchini marekani kuliko mtandao wa kutafuta wapenzi wa Tinder ( hata mapenzi yameshindwa kuiangusha Pokemon Go)
 • kwa siku mbili Gemu hii inakaribia kuipita Twitter ya Android kwa watumiaji hai wanaotumia mtandao huu kwa siku.
 • Nintendo ambao ndiyo wachapishaji wa gemu hilo tayari hisa zao zimepanda kwa kasi kubwa na kuongezea thamani ya dola za kimarekani bilioni 7.
 • Watu wanatumia mara mbili zaidi ya muda wanaotumia katika mitandao ya kijamii kama snapchat
INAYOHUSIANA  Tegemea Mambo Haya Katika Toleo La iOS 11! #MaelezoNaPicha

pokemon go

Changamoto hazikosekani katika jambo na Pokemon Go inakutana na changamoto zifuatazo

 • Kuelemewa kwa server; hii inatokana na kwamba watengenezaji hawakutegemea kuwa na watumiaji wengi hivi hii imesababisha watumiaji wengi kupatashida kucheza gemu vizuri kwasababu server zinazidiwa.
 • Gemu inakula chaji ya simu saana; Hii inatokania na ukweli kwamba game hii inatumia virtual reality ingawa unaweza kutatua hili kwa kwa kushusha ramani ya google katika simu yako kwa matumizi ya offline.
 • Vibaka nao pia wamekuwa wakikamata fursa zilizoletwa na gemu hili, kumekuwa na ripoti kwamba vibaka wamekuwa wakiwavizia watu ambao wanacheza gemu hili na kuwapora mali zao.
INAYOHUSIANA  AppStar Kutoka Vodacom, Watengenezaji wa Apps Mpo?

Ingawa gemu hili bado halijaja Tanzania lakini unaweza kulishusha na kucheza kwa kushusha toleo la APK ama kwa watumiaji wa iOS wanaweza kushusha app hii kwa kutengeneza akaunti ambayo nchi utaweka Marekani.

Kama umekwisha ijaribu Pokemon Go tuambie mtazamo wako!

 

Facebook Comments

Sambaza
1 Comments
Share
Tags: , ,

Nickson

1 Comments

 1. Hillary Clinton akamata fursa ktk gemu la Pokémon Go - TeknoKona
  July 18, 2016 at 11:00 pm

  […] Soma Zaidi: Pokemon Go: Gemu Tishio kwa mitandao ya kijamii […]