fbpx

Android, apps, Teknolojia, WhatsApp Beta

Uwezo wa DAIMA kunyamazisha vitu kwenye WhatsApp

uwezo-wa-daima-kunyamazisha-vitu-kwenye-whatsapp

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Sambaza

Katika hali ya kawaida kabisa unaweza ukawa ni mwenzangu wa kupenda viwe vinaingia kimyakimya kwenye WhatsApp bila ya sauti kusikika (kunyamazisha) lakini kwa miaka kadhaa kipengele hicho kimekuwa na ukomo!

Sina shaka kuna mawasiliano ya watu/makundi ya kwenye WhatsApp umeweka jumbe ziwe zinaingia bila ya wewe kutokuwa na taarifa lakini kipengele hicho ukikiruhusu basi kinaweza kudumu kwa saa 8, wiki moja au mwaka mzima, si ndio? Basi hilo lipo mbioni kubadilika na sasa mtu ataweza kuchagua kipengele cha “Daima kunyamazisha” taarifa fupi kwenye WatsApp (always mute); kukata sauti mara mtu anapokutumia ujumbe/jumbe zinazotumwa kweneye kundi husika.

Kwenye WhatsApp Beta 2.20.201.10 kipengele cha kuweza kuyamazisha taarifa bila ya ukomo wa muda.

Kipengele hiki kimekuwepo kwa miaka mingi tuu lakini pengine kuna wengine hawajui jinsi ya kukiruhusu kwenye simu zao. Iwapo unataka kunyamazisha (kutosikia mlio) unapotumiwa ujumbe kutoka kwa mtu basi unabofya namba/jina kwenye uwanaja wa kuandika ujumbe ndani ya WhatsApp. Utaweza kuona picha (kama ameweka) kwa ukubwa zaidi lakini wewe bofya kwenye kipengele cha “Mute” kuweza kuruhusu kutosikia mlio iwapo mhusika atakutumia ujumbe au jumbe za kwenye kundi fulani.

kunyamazisha
Peleka kwenda kulia kitufe cha “Mute notifications” ili kuweza kuzuia kusikia mlio wa ujumbe kutoka kwa mtu/kundi.

Mbali na kitu hicho kipya pia imeonekana WhatsApp Beta wanafanyia maboresho ya muonekano wa kiasi cha memori ambacho WhatsApp pamoja na vitu vingine vimechukua kwenye simu janja.

INAYOHUSIANA  Ijue Spark 2 simu mpya kutoka Tecno
kunyamazisha
Mabortesho ya kwenye WhatsApp Beta kuhusu muonekano wa tofauti kuhusu jinsi diski uhifadhi ilivyotumika.

Mara nyingi (kama si daima) maboresho ya programu tumishi yenye watumiaji wengi huanzia kwenye WhatsApp Beta kisha wengine ndio wanafuata. Hivyo, kama una simu ya Android nakushauri utumie WhatsApp Beta na uwe unakuwa masasisho kila yanapokuwepo kuweza kupata maboresho hayo mapema kabisa.

Chanzo: Gadgets 360

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Reply your comment

Your email address will not be published. Required fields are marked*