Huduma maarufu ya kuchati na kupiga simu ya Skype katika kuboresha zaidi teknolojia wameleta uwezo wa watu wanaopigiana simu au kuchati kutumia lugha tofauti kuelewena moja kwa moja bila kubadilisha lugha zao.
Kupitia teknolojia hiyo kwa mfano mmoja anaweza akawa anaandika au kuongea kijerumani na mwingine akawa anazungumza/kumjibu kwa kiingereza na watu hawa wakaelewana moja kwa moja kwani kwa yule anazungumza kutumia kijerumani atasikia majibu yakitolewa kwenye kijerumani japo kuwa anayezungumza naye amejibu kwa kiingereza.
Kuwezesha teknolojia hii itabidi uchague lugha yako na yule unayempigia. Ukizungumza sentensi flani katika lugha yako basi teknolojia hii itatafsiri na kuizungumza kupitia sauti ya kikompyuta na si yako kwa mtu husika aliyeupande wa pili wa mazungumzo hayo.
Kwa sasa uwezo wa kutafsiri maongezi upo kwa mazungumzo ya kati ya kiingereza na kiispaniola, na Sykpe wamesema wanafanya kazi kuleta teknolojia hiyo kwa lugha nyingi zaidi. Ila kwa upande wa kuchati teknolojia hii inafanya kazi kwa zaidi ya lugha 40. Bado hatujapata uhakika wa Kiswahili kuwa moja ya lugha hizo, tutakufahamisha tutakapopata uhakika.
Skype inayomilikiwa na Facebook imejikuta katika ulazima wa kujitahidi kuonesha ubora wa juu na kuwapa watumiaji sababu ya kuendelea kuitumia kwani ushindani umekuwa mkubwa sana katika eneo hilo. Kwa watumiaji wa kawaida upatikanaji wa huduma zingine kama Viber, WhatsApp na Facebook Messenger zinazotoa huduma kadhaa kama zake utumiaji wa Skype umeporomoka zaidi.
Kwa sasa huduma hii inapatikana kwa wale ambao wanashindwa kusubiria ujio rasmi, unaweza kujiandikisha hapa kuweza kuipata – (Bofya – Skype Translator), kwa sasa inafanya kazi kwenye kompyuta za Windows 8.1 na Windows 10 Preview
Tazama video elekezi kutoka Skype hapa chini;
No Comment! Be the first one.