Muda mwingi Apple imeripotiwa ikiwa ina mpango wa kutoa Macbook ambayo ina kioo kikubwa –pengine kuliko macbook zingine—na sasa ndio mwaka wa jambo hilo kuwezekana.
Apple ni moja kati ya makampuni mamkubwa sana ya teknolojia ambayo yanajitahidi mara kwa mara kuwapa wateja wake kile wanachokitaka na sasa wanafanya hiyo kupitia MacBook.
Kompyuta hii ambayo inakuja inategemewa kuja na kioo cha inchi 15.5 na ni muendelezo wa matoleo ya macbook Air na itatoka mwanzoni mwa mwezi wa nne.
Japokuwa fununu zinasema kuwa uzalishaji bado unaendelea lakini usije kushangaa kampuni inaanza kutangaza uwekaji wa oda wa mwanzoni kabisa (pre-orders) hivi karibuni.
Kwa sasa macbook zilizopo ni kwamba zina ukubwa wa kioo cha inchi 13 na hii inayokuja ikitoka ndio itakua ambayo ina kioo kikubwa zaidi.
Mpaka sasa bado sifa za undani za kompyuta hii kutoka Apple bado hazijawekwa wazi, pengine mpaka siku ya uzinduzi ndio mambo yatakua hadharani.
Vile vile Apple imesemekana ikiwa katika mchakato wa utengenezwaji wa chip (shipset) nyingine ambalo ni toleo la mbele la M2, yaani M3.
Kama unakumbuka vizuri kipindi cha zamani ni kwamba Apple walikua wameamua laptop zao za Air zilikua ni nyepesi na zinazowezekana kubebeka kiurahisi kabisa.
Na zile za Pro zilikua ni za saizi kubwa na hata matumizi yake yalikua ni makubwa kulinganisha na matoleo ya Air lakini kwa sasa Apple wanaamua kuwa sababu hizo mbili zisitenganishe matoleo yao ya kompyuta mpakato.
Ningependa kusikia kutoka kwako, je unadhani Macbook hiyo itakua na sifa za undani za aina gani? Niandikie hapo chini katika uwanja wa comment.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.