fbpx

Mwandishi wa habari wa kwanza ambae si binadamu

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Matumizi ya rasilimali watu katika kufanya shughuli mbalimbali zikitafutiwa mbadala wake na kwa sasa teknolojia ambayo inayotumiwa kwa nguvu ni ‘Utashi usio halisi‘ ambapo kwa mara ya kwanza ametambulishwa mwandishi wa habari wa kwanza duniani ambae si binadamu.

Katika hali ya kuishangaza duniani hasa waliopo kwenye sekta ya habari (kwa mtazamo wangu) nchini Uchina Nov, 9 2018 waliweka historia ya kumtambulisha mwanahabari ambae kwanza si binadamu, anatumia utashi ambao sio halisi (Artificial Intelligence) na ana uwezo wa kufanya kazi kwa saa 24, siku 365 katika mwaka.

ambae si binadamu

Mwandishi wa habari wa kwanza duniani ambae si binadamu.

Mwanahari huyo ambae ndipo teknolojia inapoelekea kwa sasa na binafsi nikiamini kuwa wanaotafuta/watangazaji habari wanaweza kukosa kazi kwa sababu kuu mbili; uwezo wa kufanya kazi kila leo lakini pia kuweza kuzungumza lugha mbalimbali (zaidi ya moja).

Wakati wa uzinduzi wa wanahabari hao mmojwapo alitangaza kwa Kichina na mwingine akatangaza kwa lugha ya Kiingereza. Pia mwanahabari huyo anaweza kunakiliwa katika matukio tofauti tofauti kuleta habari.

ambae si binadamu

Mwanahabari amabae si bindamu wakato wa utambulisho.

Wakati wa kutangaza habari kwenye shirika moja huko Uchina mwanahabari huyo alijinasibu kuwa ikiwa kitu kipo katika maandishi basi anaweza kutangaza kama mtangazaji.

Vyanzo: The Guardian, CNBC

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Nubia Red Magic 3 kuzinduliwa Aprili 28
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.