Wanasayansi nchini Marekani wamekuja na roboti mdogo wa kusaidia kuondoa vitu vidogo vyenye madhara pale vinapomezwa bahati mbaya na binadamu, na ata pia kuweza kutumika kufanya matibabu ya upasuaji wa ndani kwa ndani. Roboti huyo anamezwa kama unavyomezwa dawa ya vidonge. .

Hivi unajua kitu kama vile betri za saa za mkononi pale zikimezwa na binadamu bahati mbaya zinaweza kuwa na madhara makubwa sana? Iwe imetokea hilo au ata kama kuna michubuko, uvimbe n.k katika njia ya tumbo basi roboti huyu ataweza kutumika kuondoa kitu na ata kufanya matibabu ya ndani kwa ndani.
Inasemekana kila dakika tatu kuna mtoto mdogo mmoja amekuwa amemeza betri dogo – la saa n.k, matatizo makubwa ya kiafya yanayoweza sababisha kifo yanatokea pale betri hizo zikivujisha kemikali zilizo ndani yake.
Matatizo haya ni pamoja na kuungua kuta za u/tumbo, kuvuja damu ndani kwa ndani na ata kifo.
Teknolojia hii imetengenezwa kwa ushirikiano baina ya wanasayansi na watafiti wa chuo cha MIT nchini Marekani, Chuo cha Sheffield cha nchini Uingereza, na chuo cha teknolojia cha jijini Tokyo Japani. Roboti huyu ni mdogo sana na anamezwa akiwa amewekwa kwenye kidude kidogo cheche ukubwa wa kama vidonge vya rangi mbili.
Ataweza;
- Kushona michubuko
- Kuweka dawa eneo la kidonda cha ndani ya mfumo wa tumbo
- Kuondoa vitu visivyoitajika tumboni
Roboti huyo akiwa tumboni ataweza tembea na ata kuogelea kwenye maeneo ya majimaji. Ataweza kuongozwa na daktari kuhusu sehemu za kwenda kupitia teknolojia ya sumaku (magnetic). Ingawa roboti huyo katengenezwa na kielktroniki atakuwa salama katika maeneo ya maji maji kutokana na sehemu zake zote kufunikwa na ngozi spesheli kama ile inayotumika katika ufungaji wa ‘sausages’.
Watu wanaomeza kwa bahati mbaya mabetri yanayoleta madhara kwao hawataitaji kufanyiwa oparesheni kubwa tena kupitia teknolojia hii. Kwa sasa inaendelea kufanyiwa majaribio kabla ya kupata baraka za vyombo vya afya na kuanza kutegemewa kuanza kupatikana mahospitalini.
TAZAMA VIDEO INAYOMUONESHA ROBOTI HUYO
Je una mtazamo gani juu ya teknolojia hii?
Vyanzo; Cnet na mitandao mbalimbali
One Comment
Comments are closed.