fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
apps Mtandao Spotify Teknolojia

Kwaheri Stesheni Za Redio (Spotify Stations) Kutoka Spotify!

Kwaheri Stesheni Za Redio (Spotify Stations) Kutoka Spotify!

Spread the love

Tumeshawahi kundika mengi sana kuhusiana na mtandao wa Spotify, pitia kidogo hapa. lakini hivi unajua kuhusu Spotify Stations?

Spotify Stations ni huduma ya redio kutoka katika mtandoa wa muziki wa Spotify. Huduma hiyo ina App tofauti kabisa na App ya spotify ile ya kawaida ile tuliyoizoea.

Stesheni Za Spotify (Spotify Stations) Katika Simu Ya Android!

Stesheni Za Spotify (Spotify Stations) Katika Simu Ya Android!

App hii ilikua mahususi kwa ajili ya vipindi vya redio na ilizalishwa mwaka 2018 na kwa sasa mtandao huo umeamua kuachana kabisa na huduma hiyo.

Kinachofanyika hapa ni kwamba inafungia huduma zote za ki’App na zile za kimtandao kabisa, mpaka kufikia mwezi wa 5 tarehe 16,2022.

Mpaka sasa bado kampuni haijaweka wazi sababu za kuachana na App hiyo, lakini imesema inarudisha stesheni za redio katika App ya Spotify amabyo imezoeleka ili watu waendelee kusikiliza.

SOMA PIA  Yafahamu Majukwaa ya kujifunzia Mtandaoni

Hapa kinachofanyika ni kwamba, mtandaoni huduma hii haitapatikana, App yake haipatikani tena katika soko la App la Playstore, lakini kama bado una App katika simu unaweza ukaitumia pengine mpaka tarehe 16.

Ningependa Kusikia Kutoka Kwako, Niambie Hapo Chini Katika Uwanja Wa Comment, Taarifa Hii Umeipokea Vipi?

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii

SOMA PIA  Teknolojia ya FaceID kwenye iPhone X 'yamvuruga' John Cena

Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania