fbpx

Samsung yaonyesha simu yake ya mkunjo itakavyokuwa

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Baada ya kuandikwa sana kuhusu taarifa za Samsung kuja na simu yake ya mkunjo, hatimae kionjo cha namna simu hiyo itakavyokuwa na muonekano wake umeonyeshwa rasmi.

Kidokezo hicho cha muonekano wa simu janja ya mkunjo kutoka Samsung umeonyeshwa kwenye mkutano wa mwaka wa wakuzaji wa bidhaa za Samsung 2018 (SDC 2018) uliofanyika huko San Francisco, Marekani.

simu yake ya mkunjo

Ikikunjwa itakuwa na muonekano wa simu janja.

Hii ni ahadi iliyotolewa mwezi uliopita katika jiji la Kuala Lumpur wakati wa uzinduzi wa Galaxy A9, na DJ Koh, rais na Kkiongozi Mkuu Mtendaji wa Samsung kitengo cha simu za mkononi.

Simu hiyo ya Mmkunjo itakuwa na muunganiko wa bidhaa mbili kwa pamoja ambazo ni tabiti na simu janja. Ikikunjuliwa itakuwa na muonekano wa tabiti na ikikunjwa itakuwa na muonekano wa simu janja.

simu yake ya mkunjo

Pale itakapokuwa kunjuliwa na kuwa na muonekano wa Tabiti kioo chake kitakuwa na ukubwa wa inchi 7.3 na itakapokunjwa kioo chake kitakuwa na ukubwa wa inchi 4.6.

Itakapokuwa kwenye muonekano wa tabiti mtumiaji atakuwa na uwezo wa kufungua vitu mbalimbali kwa wakati mmoja na itaingia sokoni mwaka 2019.

Uhakika ni kwamba simu hiyo Angalia video fupi ya muonekano wa simu ya mkunjo kutoka Samsung hapo chini.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Samsung Galaxy Fold: Simu inayojikunja Kioo Kuuzwa Rasmi Aprili 26
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.