Kompyuta za magemu hutumika na watu kuchezea magemu pamoja na kutengenezea magemu. Kompyuta hizi za magemu huwa na bei kubwa kutokana na uwezo wake mkubwa unaohitajika ili kufanya kazi kwa ufanisi. Pia kompyuta hizi zinapatikana katika hali mbalimbali ikiwemo kama kompyuta mpakato (Laptop) na kama kompyuta ya mezani (Desktop).
Makampuni yanayotengeneza kompyuta hizi za magemu ni pamoja na kampuni ya Alienware, Origin PC, Lenovo na Digital Storm. Tofauti kubwa iliyopo kati ya kompyuta za magemu na kompyuta za kawaida ni kwamba kompyuta za magemu huja na kadi bora za picha za hali ya juu (GPU) pamoja na kuwa na prosesa zenye uwezo mkubwa. Mambo ya kuzingatia unapotaka kununua kompyuta kwaajili ya kuchezea magemu ni pamoja na:
Uwezo wa prosesa (CPU): Kompyuta za magemu huhitaji uwezo mkubwa wa prosesa ili kuweza kufanya kazi kwa ufanisi zaidi. Kuna aina mbili tofauti za prosesa zilizo zoeleka katika kompyuta za magemu ambazo ni Intel Core pamoja na AMD Ryzen. Ili uweze kucheza gemu za kisasa bila shida yoyote ile unashauriwa kuwa na kompyuta yenye prosesa yenye kiwango cha Intel Core i7 kwenda juu au AMD Ryzen 7 kwenda juu.
Kadi ya Picha (GPU): Hii ni aina ya prosesa maalumu kwaajili ya utengenezaji pamoja na uonyeshaji wa picha na video katika kiwago cha hali ya juu. Katika uchezaji wa magemu kompyuta inahitaji kuwa na uwezo mkubwa wa kuonyesha picha na video za gemu hilo ili kumjengea uhalisia mchezaji. Kiwango cha chini cha kadi ya picha kwa kompyuta ya magemu ni NVIDIA GeForce GTX 1060.
RAM: Kwa kompyuta za magemu unashauriwa kuwa na angalau RAM ya 16GB ili uweze kucheza magemu vizuri bila kuichosha kompyuta yako wala kuifanya kompyuta kuwa nzito.
ROM: Kwasababu magemu huchukua nafasi kubwa kwenye kompyuta unatakiwa kuwa na angalau GB 100 kwaajili ya kuhifadhia gemu lako pamoja na kumbukumbu mbalimbali zinazoambatana nayo.
Baadhi ya kompyuta za magemu ni kama Alienware Aurora Ryzen, Alienware Aurora R12, CyberPowerPC Infinity X109 na HP Omen.
No Comment! Be the first one.