fbpx
Samsung, simu, Teknolojia

Samsung Galaxy A9 ya mwaka 2018

samsung-galaxy-a9-ya-mwaka-2018
Sambaza

Samsung wameamua kupiga hatua kwenye vita ya ushidani kwa biashara ya simu rununu, Samsung Galaxy A9 ya mwaka 2018 ni ya utofauti sana wa aina yake.

Simu hiyo ambayo imetoka chini ya saa 24 zilizopita ina sifa nyingi nzuri lakini iliyotokea kuchukua vichwa vya habari ni idadi ya kamera ilizonazo katika sehemu moja. Sifa zake ni kama ifuatavyo:-

Kamera.

Hata mimi binafsi Samsung wamenivutia baada ya Galaxy A7 kuwa na kamera 3 nyuma, hii ya sasa hivi ina kamera nne (4) nyuma zikiongozwa na yenye MP 24, nyingine zikiwa na MP 8, MP 10 na MP 5 mtawaliwa. Upande wa mbele ipo moja ya MP 24.

INAYOHUSIANA  Wanyama kuweza kubashiri tetemeko la ardhi. #Sayansi
Galaxy A9 ya mwaka 2018
Idadi ya kamea (upande wa nyuma); kwa ujumla kuna kamera tano.

Kipuri mama+Muonekano.

Kupuri kilichowekwa ni Exynos 7885 kasi yake ni 4x 2.2GHz + 4x 1.8GHz. Ukubwa wa kioo ni inchi 6.3 (1080*2220pxSuper AMOLED Full HD+.

Memori ya ndani+RAM.

Samsung Galaxy A9 ina RAM GB 6 au 8/GB 128 upande wa diski uhifadhi lakini pia ina sehemu ya kuweka memori ya nje mpaka GB 512.

Betri+Programu endeshi.

Samsung wameweka Android 8 huku mategeo ya simu hiyo kupokea masasisho ya Android 9 Pie ni mpaka mapema mwakani. Kwenye upande wa betri ina 3800mAh.

INAYOHUSIANA  Uundaji wa iPhone 12 unaendelea kama kawaida

Rangi, Bei+Menngineyo.

Samsung Galaxy A9 2018 zipo zenye rangi Nyeusi, Bluu na Udhurungi huku bei yake ikiwa karibu $720|Tsh. 1,656,000. Mbali na hapo simu hiyo ina uwezo wa kujigawa kioo na kufanya kazi mbili tofauti lakini haina teknolojia ya kuchaji bila kutumia waya, huduma za Samsung Pay, Health na Bixby zipo.

Galaxy A9 ya mwaka 2018
Rangi zinazopatikana kwenye simu mpya kutoka Samsung pamoja na teknolojia ya kutumia kidole ipo upande wa nyuma.

Hiyo ndio Samsung Galaxy A9 ya mwaka 2018 ambayo inatazamiwa kuingia sokoni mwezi ujao.

Vyanzo: GSMArena, Tech Radar

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|