Mgonjwa napoenda hospitalini kwa ajili ya matatizo ya macho daktari wa macho ndio kimbilio lake lakini miaka inakwenda na teknolojia inakuwa, sasa mashine una uwezo wa kubaini magonjwa ya macho.
Kikundi kinachofahamika kama DeepMinds wametengeneza mashine inayotumia “Werevu wa kufikirika” (Artificial Intelligence) na kwa ushirikiano wa madaktari kutoka hospitali ya macho ya Moorfields wamethibitisha kuwa kifaa hicho kina uwezo wa kutambua magonjwa ya macho kwa ufasaha kabisa unafikia 94%.
Hatua inazopitia kifaa hicho ni mbili ambapo inaangalia retina kwenye jicho la mgonjwa kisha baada ya hapo kile ilichokibaini kinapitishwa kwenye mashine tano tofauti kabla ya kutoa majibu kamili.
Kifaa hicho pia kinaweza kutoa kipaombele kulingana na tatizo la mgomjwa na hivyo kufanya mlengwa kupatiwa matibabu kwa haraka hatimae kuondoa uwezekano wa kupoteza uwoni.
Kwa sasa kifaa hicho bado hakijaanza kutumiwa lakini hatua inayofuata ni kufanyiwa majaribio kwenye hospitali mbalimbali pamoja na kupewa kibali baada ya mamlaka husika nchini Uingereza kukiidhinisha.
Chanzo: The Guardian