LG ni kampuni kubwa la mambo ya elektroniki ambalo lipo nchini Korea. Kwa sasa kampuni imejiweka katika hali nzuri (kujikuza) baada ya kuweka sokoni simu ambazo zimetengenezewa kutoka india.
Kampuni limeweka alama ya aina yake baada ya kuzalisha simu za K7 na K10.
“ Hatujapata simu ambazo zinafanya vizuri katika soko la huku mpaka sasa. Lakini tunaamini kuwa biashara nzima ya simu itaanza kuwekewa mkazo na kukuzwa na kampuni” – Alisema Bw. Kim Ki-Wan mkuu wa LG ya India
Kampuni imeongezea kuwa ina tegemea simu janja ziweze kuchangia asilimia 10 ya mapato yota mpaka mwaka ujao. Kampuni kuanza kutengeneza simu zake za LG ambazo kila kitu kinafanyikia India ni moj akati ya hatua ili kuhakikisha mafanikio yanapatikana
Kampuni mpango wake ni kuuza simu milioni moja ndani ya India peke yake. Pia LG inaweza ikaongezea bidhaa zingine katika soko ambazo sio simu janja. Licha ya hivyo LG sio lazima iuze simu janja tuu ambazo imezizalisha ndani ya nchi (zinaweza hata zikatoka nje) ila kampuni litahakikisha limezalisha simu nyingi ndani ya nchi
Ukiachana na simu janja bidhaa zingine ambazo LG wanaweza wakaipatia India ni Tv janja (Smart TV). TV hizi au hata zile zijulikanazo kama ‘OLED TVs’ sina soko kubwa sana katika nchi ya India. Kampuni limeotea kuwa nchi inauhitaji mkubwa sana wa TV janja.
India ni moja kati ya nchi ambazo zimewekewa malengo makubwa sana na kampuni mama ya LG na pia kampuni inaamini kuwa nchi hiyo ina fursa nyingi sana ukilinganisha na nchi zingine nyingi tuu