Ni wazi kuwa makampuni ambayo yanajihusisha kabisa na teknolojia huwa kuna muda yanauzwa au hata kununuliwa kwa dau kubwa sana, leo tunakuletea orodha ya makampuni yalionunuliwa kwa dau kubwa kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita
Mfano mzuri ni mtandao ya kijamii ikiwa inauzwa au kununuliwa mara nyingi inakua inahusisha hela nyingi sana, Leo tutaangazia makampuni 10 ya teknolojia ambayo yamenunuliwa kwa pesa nyingi kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita. HII NI SEHEMU YA PILI
2019: IBM Iliinunua Red Hat Kwa Dola Za Kimarekani Bilioni 34.
IBM ni moja kati ya makampuni ya zamani na yanajihusisha moja kwa moja na teknolojia, kuna wengine wanaijua IBM kama kampuni ambayo inahusika moja kwa moja na uzalishaji wa kompyuta na vifaa vyake.
Mwaka 2019, kampuni hiyo iliinunua kampuni ya Red Hat ambayo inajihusisha moja kwa moha na uzalishaji wa Software ambazo ziko wazi kwa jamii (Open-Source software)
2016: SoftBank Iliinunua Arm Kwa Dola Za Kimarekani Bilioni 31.4
SoftBank ni kampuni ya kijapani ambayo imejikita sana katika uwekezaji na iliinunua kampuni ya Arm mwaka 2016. Japokua Arm imekua sana tangia kipindi hicho lakini bado Softbank ina mpango wa kuiuza kampuni hiyo mwaka 2023.
2020: Salesforce Iliinunua Slack Kwa kiasi Cha Dola Bilioni 27.7 Za Kimarekani.
Slack ni mtandao wa mawasiliano na mara nyingi unatumika na timu (mfano Timu nzima ya TeknoKona tunaweza kujumuika na kuwasiliana).
Kampuni hiyo ya mawasiliano mara nyingi kwa njia ya meseji ilinunuliwa na Salesforce mwaka 2020. Kingine ni kwamba Salesforce wanategemea Slack kushindana vikali na Microsoft Teams ambayo imekua kwa kasi na kujipatia umaarufu tangia UVIKO 19 kuitafuna dunia
2016: Microsoft Iliinunua Kampuni Ya LinkedIn Kwa Dola Za Kimarekani Bilioni 26.2.
Kwa sasa LinkedIn ni kampuni ambayo iko chini ya Microsoft, LinkedIn ni mtandao wa kijamii lakini ni mahususi kwa ajili ya wafanya biashara na wafanya kazi au wataalamu na umejikita katika Netiweki.
Kwa sasa mtandao huo umeunganishwa moja kwa moja na huduma ya Office 365. Kwa kipindi hicho hili ndio likua dili la hela ndefu ambalo Microsoft imelifanya na hii ni kabla ya Activision Blizzard
2020: T-Mobile Imeinunua Sprint Kwa Kiasi Cha Dola Bilioni 26 Za Kimarekani
Sprint pia alikua ni moja kati ya washindani wakubwa wa T-mobile lakini kwa mwaka 2022 kampuni ilimnunua.
Jambo hili limeleta mabadiliko makubwa sana katika teknolojia kwa ujumla na kwa sasa marekani kuna watoaji 3 wa huduma ya mtandao (kama Tigo, Voda N.k) tuu ambao ni wakubwa Verizon,T-Mobile US na AT&T Mobility
Ni wazi kuwa makampuni ambayo yanajihusisha na Teknolojia mara nyingi huwa yanahusika na kutengeneza pesa nyingi sana katika biashara zake na vile vile sekta ya teknolojia ni sekta ambayo inaheshimika sana
Makampuni haya tajwa hapo juu mara nyingi sana watumiji wa huduma wa mwisho wanajuaga kama yanajitengemea ila ukija kuchunguza unagundua kuwa yanamilikiwa na makampuni mengine ambayo ni makubwa zaidi – lakini wakati mwingine hili halina maana sio?
SOMA SEHEMU YA KWANZA >>HAPA<<
Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika uwanja wa comment, je unadhani kuna manunuzi mengine ambayo ni makubwa na unahisi nimeyaruka?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.